Swali: Wapo baadhi ya waislamu watenda maasi ambao tunawatembelea kwa lengo la kuwalingania kwa Allaah (´Azza wa Jall). Lakini hawaji katika darsa na wako mbali na Allaah (´Azza wa Jall). Tunaona kuwa wafanya baadhi ya maovu na wakati mwingine wanatupa mtihani mfano wa kuweka TV na muziki kipindi tunapokuwa huko. Hatuwalinganii mbele ya watu wengine, tunawaendea majumbani mwao. Mwanzoni tunafanya matembezi ya kukariri ili kuwafungamanisha na sisi. Tumepata uzowefu kwamba tukianza kuwakemea maovu moja kwa moja, watakimbia mbali nasi. Baadhi ya nyakati tunasikia tunasikia baadhi ya maovu lakini tunasubiri. Baadhi ya ndugu wanayakemea na wanasema ni lazima kukemea maovu. Je, tukemee maovu papo hapo au tusubiri kwa lengo la ulinganizi?

Jibu: Mtu anayekemea maovu ni kama daktari. Pengine madhara yakawa makubwa zaidi ikiwa daktari atataka kufungua donda na kutoa yale yaliyomo ndani. Lakini badala yake ikiwa atalitunza kidogo kidogo na akavumilia ile harufu mbaya, atafikia lengo. Nyinyi hamkuketi nao kwa ajili ya kutaka maovu. Mmeketi nao ili muweze kuwalingania kwa Allaah. Nafikiria kwamba kila mtu mwenye akili akiketi karibu na mtu mwema basi ataacha kufanya maasi. Pengine akafanya kiburi au akaendelea kufanya ukaidi akaendelea kubaki alivyo au hata akawa mbaya zaidi. Subiria. Ukikata matumaini juu yake basi usiendelee kukaa naye. Katika hali hiyo ni lazima kuachana naye.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (17 A)