103. Kama nyuki anavyoizunguka ´Arshi

100 – Shurayh bin ´Ubayd alikuwa akisema:

”Kwako hupandishwa sauti ya matukuzo. Kwako yanapanda hadhi ya matakaso. Kutakasika ni Kwako Mwenye ufalme. Mkononi Mwako ndio mna enzi, ufalme, funguo na makadirio.”[1]

Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh.

101 – Ka´b amesema:

”Allaah ametakasika na mapungufu, himdi zote njema anastahiki Allaah, hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, Allaah ni mkubwa zinaizunguka ´Arshi kama nyuki na zinamtaja yule mwenye kuzitamka.”

102 – Ka´b amesema tena:

”Hakika maneno mazuri yanaizunguka ´Arshi kama azungukavyo nyuki na yanamtaja mwenye nayo.”[2]

Yote mawili yamethibiti kutoka kwa Ka´b al-Ahbaar.

[1] Abush-Shaykh (1/19). Cheni ya wapokezi ni Swahiyh kwa mujibu wa Ibn-ul-Qayyim, uk. 105.

[2] Abu Ja´far bin Abiy Shaybah katika “Kitaab-ul-´Arsh” (2/162 – muswada) kwa cheni mbili ambazo ni Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 122
  • Imechapishwa: 12/07/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy