103 – Abu Qilaabah amesema:
”Wakati Allaah (Ta´ala) alipomshusha Aadam alisema: ”Ee Aadam! Nitashusha Nyumba pamoja nawe ambayo inazungukwa kama inavyozungukwa ´Arshi Yangu. Kutaswaliwa hapo kama kunavyoswaliwa kwenye ´Arshi Yangu.” Itabaki kuwa hivo mpaka wakati wa gharika. Hivyo ikawa pindi Mitume wanapohiji mahali hapo, huiendea bila kujua mahali ilipo, mpaka pale Allaah alimpomjaalia Ibraahiym (´alayhis-Salaam) kuijenga.”
Yamethibiti kutoka kwa Abu Qulaabah. Ni nani ambaye anaweza kulinganishwa na Abu Qilaabah katika ubora na utukufu? Alikimbia kutoka ´Iraaq kwenda Shaam kwa ajili ya kufanya kazi kama Qaadhiy.
104 – Haakim bin Jaabir amesema:
”Nimekhabarishwa kwamba Mola wenu (´Azza wa Jall) hakugusan kwa mikono Yake isipokuwa tu vitu vitatu: Ameipanda Pepo kwa mkono Wake, Akamuumba Aadam kwa mkono Wake na akaiandika Tawraat kwa mkono Wake.”[1]
105 – Abu Dharr amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Ee Abu Dharr! Mbingu saba ukizilinganisha na Kursiy si kitu isipokuwa ni kama mfano wa kijipete cha chuma kilichotupwa katika uwanja mkubwa. ´Arshi ukiilinganisha na Kursiy ni kama huo uwanja mkubwa ukiulinganisha na kijipete hicho.”
Ibraahiym si chochote ingawa amefanywa kuwa madhubuti[2].
106 – Ibn ´Abbaas aliingia kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) wakati alipokuwa katika hali ya kukata roho akamwambia:
”Wewe ulikuwa ndiye mwanamke unayependeza zaidi mbele ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) – na hakuwa akipenda isipokuwa vilivyo vizuri tu. Allaah amekutakasa kutoka juu ya mbingu saba.”[3]
Ameipokea ad-Daarimiy, uk. 105, katika ”ad-Radd ´alaa Bishr Maariysiy”.
[1] Ameipokea al-Aajurriy katika ”as-Shariy´ah, uk. 303, kwa cheni ya wapokezi Swahiyh, na ´Abdullaah bin Ahmad amepokea mfano wake katika ”as-Sunnah”, uk. 68, lakini pasi na kutaja kugusa na kupanda Pepo. Mtunzi ameisahihisha katika “al-Arba´iyn fiy Swifaati Rabb-il-´Aalamîn” (2/179 – muswada). Ameisimulia pia kwa ukamilifu wake kutoka kwa ´Ikrimah kwa cheni ya wapokezi dhaifu na mfano wake kutoka kwa Khaalid bin Ma´daan. ad-Daarimiy, uk. 35, amepokea mfano wake kutoka kwa Maysarah kwa wapokezi madhubuti. Vivyo vivyo ndivo alivofanya Anas kutoka kwa Ka´b kwa cheni ya wapokezi Swahiyh ambayo pia imepokelewa na al-Aajurriy.
[2] Hata hivyo hakupwekeka katika kuisimulia, na kwa ajili hiyo ndio maana nikaitaja katika ”as-Swahiyhah” (109).
[3] Ameipokea ad-Daarimiy katika “ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah”, uk. 27-28, kwa cheni ya wapokezi Swahiyh kwa mujibu wa sharti za Muslim.
- Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 123-126
- Imechapishwa: 12/07/2024
- taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy

Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 123-126
Imechapishwa: 12/07/2024
taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
https://firqatunnajia.com/104-mwanamke-aliyekuwa-akipendwa-zaidi-na-mtume/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)