09. Msibiwaji anatakiwa alinganishe starehe ya maisha ya dunia na Aakhirah

Miongoni mwa pozo lenye kuwapoza waliopatwa na msiba ni yule msibiwaji kuangalia na kupima kati ya starehe ya maisha ya dunia hii itayoisha na starehe ya maisha ya Aakhirah yatayodumu na ni ipi katika hizo ambayo ina starehe ya milele kwa yule msibiwaji pamoja na thawabu za kusema “Sisi ni wa Allaah na Kwake ndiko tutarejea” na kuwa na subira. Atapoona ni lipi lenye uzito zaidi na akalichagua, basi amshukuru Allaah kwa hilo. Hata hivyo ikiwa atachagua hilo la pili lenye uzito khafifu katika pande zote, basi atambue kuwa msiba juu ya akili zake, moyo wake na dini yake ni khatari zaidi kuliko msiba uliosibu mambo yake ya kidunia. Ni vipi itakuwa starehe ya dunia hii ilihali Allaah (Ta´ala) anasema juu yake:

قُلْ مَتَاعُ الدُّنْيَا قَلِيلٌ

“Sema: “Starehe za dunia ni chache.””

Ni kipi anachofikia mtu katika kichache?

Mwenye kuchagua kichache na mambo ya muda juu ya makubwa na ya milele basi ni mgonjwa wa akili. Baadhi ya wenye hekima wamesema:

“Mjinga hudhania kuwa kisicho kitu ni kitu na kitu ni kisicho kitu. Asiyeacha kisicho kitu hatofikia kitu. Asiyejua kile kilicho kitu hatoacha kile kisicho kitu.”

Bi maana maisha ya dunia hii na ya Aakhirah. Haya yamesemwa na Ibn Abiy Dunyaa katika “Dhamm-ud-Dunyaa”.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 20-21
  • Imechapishwa: 13/10/2016