360 – Twaariq bin Shihaab amesimulia:

أنه بات عند سلمان الفارسي رضي الله عنه لينظر ما اجتهاده. قال: فقام يصلى من آخر الليل فكأنه لم ير الذى كان يظنُّ فذُكرَ ذلك له فقال سلمان: حافظوا على هذه الصلوات الخمس، فإنهن كفاراتٌ لهذه الجراحات ما لم تصب المقتلة

“Alilala kwa Salmaan bin Faarisiy (Radhiya Allaahu ´anh) ili aone ijtihada yake. Akasimama kuswali mwishoni mwa usiku. Ni kana kwamba hakuna kile alichokuwa anatarajia, akamweleza jambo hilo. Ndipo Salmaan akasema: “Vihifadhi vipindi vitano hivi vya swalah. Hakika ni kifutio cha madhambi haya muda wa kuwa mtu anaepuka madhambi yanayoangamiza.”[1]

Ameipokea at-Twabaraaniy katika “al-Mu´jam al-Kabiyr” kutoka kwa Swahabah kwa cheni ya wapokezi isiyokuwa na neno.

[1] Swahiyh kupitia zingine kutoka kwa Swahabah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/266-267)
  • Imechapishwa: 01/12/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy