10. Hadiyth “Anatumwa mwenye kunadi wakati wa kila swalah ambaye anasema… “

359 – Imepokelewa kutoka kwa ´Abdullaah bin Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

يُبعثُ منادٍ عند حضرة كل صلاةٍ، فيقول يا بنى آدم: قوموا فأطفئوا ما أوقدتم على أنفسكم، فيقومون فيتطهرون ويصلون الظهر فيغفر لهم ما بينهما فإذا حضرت العصر فمثل ذلك، فإذا حضرت المغرب فمثل ذلك، فإذا حضرت العتمة فمثل ذلك فينامون فمُدلجٌ في خيرٍ، ومدلجٌ في شرٍّ

“Anatumwa mwenye kunadi wakati wa kila swalah ambaye anasema: “Ee wana wa Aadam! Simameni mzime kile mlichojiwashia wenyewe!” Hivyo wanasimama, wanajitwahirisha na wanaswali Dhuhr, ambapo wanasamehewa yaliyo kati yazo. Vivyo hivyo inapofika ´Aswr. Vivyo hivyo inapofika Maghrib. Vivyo hivyo inapofika ´Atamah. Kisha, baada ya kusamehewa, wanaenda kulala mwanzoni mwa usiku. Baadhi wanaingia katika kheri, na wengine wanaingia katika shari.”[1]

Ameipokea at-Twabaraaniy katika “al-Mu´jam al-Kabiyr”.

[1] Nzuri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/266)
  • Imechapishwa: 01/12/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy