361 – ´Amr bin Murrah al-Juhaniy (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

جاء رجلٌ إلى النبى صلى الله عليه وسلم. فقال: يا رسول الله أرأيت إن شهدت أن لا إله إلا الله، وأنك رسول الله وصليت الصلوات الخمس، وأديت الزكاة، وصمت رمضان وقمته فممن أنا؟ قال: من الصديقين؟ قال: من الصديقين والشهداء

“Alikuja bwana mmoja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Ee Mtume wa Allaah! Unasemaje iwapo nitashuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na kwamba wewe ni Mtume wa Allaah, nikaswali zile swalah tani, nikatoa zakaah na  nikafunga Ramadhaan na nikaabudu nyusiku zake? Mimi nitakuwa miongoni mwa kina nani? Akasema: “Wale wakweli mno na mashahidi.”[1]

Ameipokea al-Bazzaar, Ibn Khuzaymah katika “as-Swahiyh” na Ibn Hibbaan katika “as-Swahiyh”. Tamko ni la Ibn Hibbaan.

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/267)
  • Imechapishwa: 01/12/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy