Nimefikiwa na Radd, pingamizi au karipio kutoka kwa Shaykh Abul-Hasan al-Ma´ribiy juu ya swali nililoulizwa. Muulizaji alisema:

”Swali la kwanza: Muheshimiwa Shaykh Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy (Hafidhwahu Allaah). Je, ni kweli kuwa umejirejea katika kumfanyia Tabdiy´ Abul-Hasan al-Miswriy?

Jibu: Hapana. Maneno haya si sahihi.

Kisha akasema[1]:

Maelezo juu ya jibu la kwanza. Ni kipi kilichokufanya unifanyie Tabdiy´ kwanza? Na ni kipi kilichokufanya uwe na msimamo juu ya hilo na usijirejee? Inatakikana kwa Shaykh ataje dalili ya kielimu au ya kihisia juu ya hilo. Hakuna nafasi ya kukubali kitia chumvi au madai, kama walivyoona wengi katika maneno ya Shaykh Rabiy´.”

Majibu juu ya swali hili la kwanza ni kama ifuatavyo:

Mosi ni kumtetea kwako Sayyid Qutwub na kusema kwako kwamba maneno yake ya kijumla yanatakiwa kufasiriwa kwa maneno yake yaliyopambanulia, licha ya kwamba Sayyid Qutwub amesema:

1 – Amefasiri Suurah ”al-Ikhaasw” kwa ´Aqiydah ya watu wenye kuamini kila kitu ni Allaah (وحدة الوجود)[2].

2 – Ameukufurisha ummah wa Muhamamd (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika tafsiri yake ya Suurah ”al-Hijr” na akasema:

”Hii leo hakuna juu ya uso wa ardhi nchi ya kiislamu wala jamii ya kiislamu iliyosheheni Shari´ah ya Allaah na ufahamu wa kiislamu.”[3]

3 – Amesema kuhusu Muusa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Alikuwa ni mfano wa kiongozi mwenye msukumo na mwenye kuudhika kirahisi.”[4]

Huku ni kumtukana mmoja katika wale Mitume tano bora.

4 – Amewatukana baadhi ya Maswahabah akiwemo ´Uthmaan bin ´Affaan (Radhiya Allaahu ´anh) na akaangusha chini ukhalifah wake[5].

5 – Amemtukana Mu´aawiyah na ´Amr bin al-´Aasw (Radhiya Allaahu ´anhumaa) kwa maneno mabaya na akawatuhumu:

”… vitimbi, ukhaini, udanganyifu na rushwa… ”[6]

6 – Amezipindisha maana sifa za Allaah (´Azza wa Jall) katika kila mahali alipoweza kupata sifa yoyote ya Allaah ndani ya Qur-aan. Amefasiri kulingana kwamba ni kutawala na ana matamshi mengine ambayo kwayo amefasiri uso, mikono ya Allaah na nyinginezo[7].

7 – Amesema:

”Ni lazima kwa Uislamu uhukumu kwa sababu ndio ´Aqiydah pekee iliyojengeka ambayo inaunda mchanganyiko kamili wa ukristo, ukomunisti ambayo iko na malengo ya vyote hivyo viwili na ukiongezea usawa, maelewano na ukatikati.”[8]

Hii ni kufuru kwa sababu amefanya Qur-aan inatokana na itikadi ya ukristo iliyopotoshwa na ukomunisti wakanamungu. Amesahau kuwa Qur-aan ni Wahy kutoka kwa Allaah.

8 – Amesema kuwa misikiti ni mahekalu ya kipindi cha washirikina pasi na kubagua chochote[9].

Unamtetea licha ya majanga yote haya na mengine zaidi. Kutoyakemea ni dalili ya wazi kabisa kwamba unawatetea kwa nguvu kabisa wazushi bila kujali Bid´ah zao ni ukafiri au za maovu. Hilo ni kutokana na kukinaika kwako na maneno yao. Hili tu linatosha kukuzingatia wewe kama mzushi.

[1] Abul-Hasan.

[2] Fiy Dhwilaal-il-Qur-aan (6/4006).

[3] Fiy Dhwilaal-il-Qur-aan (4/2122).

[4] at-Taswiyr al-Fanniy fiyl-Qur-aan, uk. 152.

[5] al-´Adaalah al-Ijtimaa´iyyah, uk. 206.

[6] Kutub wa Shakhswiyyaat, uk. 242.

[7] Fiy Dhwilaal-il-Qur-aan (3/1762-1763).

[8] Ma´rakat-ul-Islaam war-Ra’smaaliyyah, uk. 61.

[9] Fiy Dhwilaal-il-Qur-aan (3/1816).

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tanbiyh al-Wafiy ´alaa Mukhaalafaat Abiyl-Hasan al-Ma’ribiy, uk. 285-290
  • Imechapishwa: 01/12/2022