Pili ni kwamba unamtetea al-Maghraawiy ambaye ni Takfiyr na anakufurisha kwa madhambi. Hivo ndivo yanadhihirisha maneno yake. Anaita madhambi yanayofanywa na waislamu kuwa:

“… ni kama uabudiaji ndama kama ndani ya wana wa israaiyl. Utiifu katika kumuasi Allaah ni uabudiaji sanamu.”[1]

Ina maana kwamba yule mwenye kumtii mtu amemfanya kuwa sanamu. Unamtetea na kusema:

“Anapozungumzia uabudiaji ndama na uabudiaji sanamu anaingia kwa ndani. Anapozungumza kwa baadhi ya matamshi ambayo udhahiri wake ni kuwakufurisha watenda madhambi, lau ningelikuwa simjui vyema Shaykh al-Maghraawiy, basi ningesema kuwa anakufurisha kwa madhambi. Ningesema hivo laiti ingelikuwa simjui, lakini mimi namjua. Kwa ajili hiyo mimi nafasiri maneno yake ya kijumla kutokana na ile ´Aqiydah yake ya wazi ninayoitambua wakati ninapozungumza naye. Hii ndio kanuni ambayo mimi naitambua, ya kwamba maneno ya wanamme yaliyokuja kwa jumla yanafasiriwa kwa maneno yao yaliyopambanuliwa.”[2]

Umesema wakati ulipokuwa ukimtukuza na kumkweza al-Maghraawiy:

“Nitawezaje kuondoa mlima na kusimamisha wakulima wa nyanya?”[3]

Hivyo ndivyo unaafikiana na wazuhi pindi unapowasifu, unawatapa na kukubaliana nao sambamba na kwamba unawajengea chuki Salafiyyuun na kuwatukana.

[1] Kaseti ”Mawaaqifu Ibraahiym” (3).

[2] Kaseti ”Munaaqashatu Ma’rib”.

[3] Kaseti ”Haqiyqat-ud-Da´wah” (2).

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tanbiyh al-Wafiy ´alaa Mukhaalafaat Abiyl-Hasan al-Ma’ribiy, uk. 290-291
  • Imechapishwa: 01/12/2022