32. Hivi ndivo wanavoamini watu wa maoni (أهل الرأي)

Watu wa maoni (أهل الرأي). Ni wazushi na wapotofu na ni maadui wa Sunnah na mapokezi. Wanaona dini kuwa ni maoni, vipimo na mambo wanayoonelea kuwa mazuri. Wanaenda kinyume na mapokezi, wanazibatilisha Hadiyth, wanamrudi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wanamfanya Abu Haniyfah na wenye kuonelea maoni yake kuwa ndio maimamu wao; wanaabudu kwa dini yao na wanasema yale wanayoyasema. Kuna upotofu gani ulio wazi kushinda wa ambaye anaona hivi au akafuata mfumo huu na akaacha maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake na badala yake akafuata maoni ya Abu Haniyfah na wafuasi wake? Haya pekee yanatosha kuwa ni upotofu, kuchupa mpaka na kutupilia mbali.

  • Mhusika: Imaam Harb bin Ismaa´iyl al-Kirmaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Sunnah, uk. 94-95
  • Imechapishwa: 02/12/2022