08. Hadiyth “Allaah ana Malaika ambaye anaita wakati wa kila swalah… “

358 – Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

إن لله ملكاً ينادى عند كل صلاةٍ: يا بنى آدم قوموا إلى نيرانكم التى أوقدتموها فأطفئوها

“Allaah ana Malaika ambaye anaita wakati wa kila swalah: “Ee wana wa Aadam! Simameni kuelekea katika Moto wenu, mliouwasha, na hivyo uzimeni!”[1]

Ameipokea at-Twabaraaniy katika “al-Mu´jam as-Swaghiyr” na “al-Mu´jam al-Awsatw”. Yahyaa bin Zuhayr al-Qurashiy ameisimulia peke yake. Wapokezi wengine wametajwa katika yale mapokezi ya kwanza Swahiyh.

[1] Nzuri na Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/265)
  • Imechapishwa: 01/12/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy