356 – ´Abdullaah bin Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

تحترقون تحترقون ، فإذا صليتم الصبح غسلتها، ثم تحترقون تحترقون فإذا صليتم الظهر غسلتها ثم تحترقون تحترقون، فإذا صليت العصر غسلتها، ثم تحترقون تحترقون، فإذا صليتم المغرب غسلتها، ثم تحترقون تحترقون، فإذا صليتم العشاء غسلتها، ثم تنامون، فلا يكتب عليكم حتى تستيقظوا

“Mnaungua[1], mnaungua; mnaposwali swalah ya asubuhi, yanaoshwa. Kisha mnaungua, mnaungua; mnaposwali Dhuhr, yanaoshwa. Kisha mnaungua, mnaungua; mnaposwali Dhuhr, yanaoshwa. Kisha mnaungua, mnaungua; mnaposwali ´Aswr, yanaoshwa. Kisha mnaungua, mnaungua; mnaposwali Maghrib, yanaoshwa. Kisha mnaungua, mnaungua; mnaposwali ´Ishaa, yanaoshwa. Baada ya hapo mnalala – na hakuna kitu mnachoandikiwa mpaka pale mnapoamka.”[2]

Ameipokea at-Twabaraaniy katika “al-Mu´jam as-Swaghiyr” na “al-Mu´jam al-Awsatw” kwa cheni ya wapokezi nzuri. Ameipokea pia katika “al-Mu´jam al-Kabiyr” kutoka katika maneno ya Swahabah, kitu ambacho sahihi zaidi. Wapokezi wake wametajwa katika yale mapokezi ya kwanza Swahiyh.

[1] Bi maana maangamia kutokana na wingi wa madhambi.

[2] Nzuri na Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/265)
  • Imechapishwa: 01/12/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy