08. ´Ibaadah aliyotakasiwa Allaah nia

Allaah (Ta´ala) amesema kuhusu kumtakasia Yeye nia:

وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ حُنَفَاء

“Hawakuamrishwajengine isipokuwa wamwabudu Allaah hali ya kumtakasia Yeye dini kwa kujiengua na shirki na kuelemea Tawhiyd.”[1]

إِنَّا أَنزَلْنَا إِلَيْكَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ فَاعْبُدِ اللَّـهَ مُخْلِصًا لَّهُ الدِّينَ أَلَا لِلَّـهِ الدِّينُ الْخَالِصُ

”Hakika Sisi tumekuteremshia Kitabu kwa haki, basi mwabudu Allaah kwa kumtakasia dini Yeye.”[2]

قُلْ أَمَرَ رَبِّي بِالْقِسْطِ ۖ وَأَقِيمُوا وُجُوهَكُمْ عِندَ كُلِّ مَسْجِدٍ وَادْعُوهُ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ

”Sema: ”Mola wangu ameniamrisha uadilifu na elekezeni nyuso zenu katika kila sehemu mnaposujudu na mwombeni Yeye kwa kumtakasia Yeye dini.”[3]

قُلْ إِنِّي أُمِرْتُ أَنْ أَعْبُدَ اللَّـهَ مُخْلِصًا لَّهُ الدِّينَ وَأُمِرْتُ لِأَنْ أَكُونَ أَوَّلَ الْمُسْلِمِينَ قُلْ إِنِّي أَخَافُ إِنْ عَصَيْتُ رَبِّي عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ قُلِ اللَّـهَ أَعْبُدُ مُخْلِصًا لَّهُ دِينِي

”Sema: ”Hakika mimi nimeamrishwa nimwabudu Allaah hali ya kumtakasia Yeye dini na nimeamrishwa kuwa niwe wa kwanza wa waislamu. Sema: ”Hakika nakhofu nikimuasi Mola wangu adhabu ya siku kuu. Sema: ”Allaah pekee namwabudu hali ya kumtakasia Yeye tu Yeye dini yangu.”[4]

فَادْعُوا اللَّهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ

 “Basi mwombeni Allaah hali ya kumtakasia Yeye dini, japokuwa wanachukiwa makafiri.”[5]

´Umar bin al-Khattwaab (RadhiyaAllaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (SwallaAllaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika si venginevyo kila kitendo kinategemea na nia na kila mmoja atalipwa kwa kile alichonuia. Hivyo basi, yule ambaye kuhajiri kwake kutakuwa kwa ajili ya Allaah na Mtume Wake basi kutakuwa kwa ajili ya Allaah na Mtume Wake. Na yule ambaye kuhajiri kwake kutakuwa kwa ajili ya dunia au mwanamke anayetaka kumuoa basi kuhajiri kwake kutakuwa kwa kile alichokihajiria.”[6]

ash-Shawkaaniy (RahimahuAllaah) amesema kuhusiana na Hadiyth hii:

“Hakuna matendo yoyote yanayofikiwa wala kuthibiti isipokuwa kwa nia. Aina zote za utiifu na ´ibaadah ni upuuzi mtupu ikiwa hazitokani na nia takasifuna dhamiri njema. Matendo kama hayo yakiwa sio maasi basi angalau kwa uchache ni upuuzi na mchezo.”[7]

[1]98:5

[2] 39:2-3

[3] 7:29

[4] 39:11-14

[5] 40:14

[6] al-Bukhaariy (1) na Muslim (1906).

[7]Adab-ut-Twalab, uk. 5

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas Aal ´Abdil-Kariym
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hujaj al-Qawiyyah ´alaa anna Wasaa-il-ad-Da´wah Tawqiyfiyyah, uk. 12-13
  • Imechapishwa: 02/05/2023