09. Ili kitendo kiweze kukubaliwa

Ufuataji umejulishwa na maneno Yake Allaah (Ta´ala):

وَأَنَّ هَـٰذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ ۖ وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ

“Hii ndio njia Yangu iliyonyooka, hivyo basi ifuateni na wala msifuate vichochoro [vinginevyo]; vikakufarikisheni na njia Yake!”[1]

اتَّبِعُوا مَا أُنزِلَ إِلَيْكُم مِّن رَّبِّكُمْ وَلَا تَتَّبِعُوا مِن دُونِهِ أَوْلِيَاءَ ۗ قَلِيلًا مَّا تَذَكَّرُونَ

“Fuateni yale mliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wenu na wala msifuate badala Yake wasaidizi wengine. Ni machache mnayoyakumbuka.”[2]

اتَّبِعْ مَا أُوحِيَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ وَأَعْرِضْ عَنِ الْمُشْرِكِينَ

”Fuata uliyofunuliwa Wahy kutoka kwa Mola wako. Hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Yeye; na jitenge na washirikina.”[3]

قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّـهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّـهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ

“Sema: “Mkiwa mnampenda Allaah, basi nifuateni mimi. Hivyo atakupendeni Allaah na atakusameheni dhambi zenu na Allaah ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.”[4]

´Aaishah (RadhiyaAllaahu ´anhaa) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yeyote atakayezua katika amri yetu hii kile kisichokuwemo kitarudishwa.”[5]

Imekuja katika upokezi mwingine:

“Yeyote atakayefanya katika amri yetu hii kisichoafikiana na amri yetu kitarudishwa.”[6]

Haafidhw Ibn Rajab (RahimahuAllaah) amesema:

“Hadiyth hii ni msingi mtukufu katika misingi ya Uislamu na inafanya kazi kama mizani ya matendo kwa uinje wake. Ni kama ambavo Hadiyth isemayo kuwa matendo yanalipwa kutegemea na nia ni mizani ya matendo kwa undani wake. Kama ambavo kila kitendo kisichofanywa kwa ajili ya Allaah basi mwenye nacho hapati thawabu zozote, vivyo hivyo kila kitendo ambacho kisichoafikiana na amri ya Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni chenye kurudishiwa yule mtendaji. Kila mwenye kuzua ndani ya dini kile ambacho Allaahhakukiidhinisha na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) basi hakina chochote kuhusiana na dini. Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “… kisichoafikiana na amri yetu… “ kuna ishara ya kwamba matendo yote ya watendaji ni lazima yawe yanaafikiana na Shari´ah. Hukumu za Shari´ah ndio zenye kuyaamua inapokuja katika maamrisho na makatazo yake. Yale matendo yanayoafikiana na hukumu za Shari´ah ndio yenye kukubaliwa, na yale matendo yasiyokuwa hivo basi ni yenye kurudishwa nyuma.”[7]

[1] 6:153

[2] 7:3

[3] 6:106

[4] 3:31

[5] Muslim (1718).

[6] al-Bukhaariy (2697).

[7]Jaamiy´-ul-´Uluumwal-Hikam (1/176-177).

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas Aal ´Abdil-Kariym
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hujaj al-Qawiyyah ´alaa anna Wasaa-il-ad-Da´wah Tawqiyfiyyah, uk. 13-14
  • Imechapishwa: 02/05/2023