Uongo ni sifa mbaya. Uongo ni miongoni mwa sifa za wanafiki. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Alama za mnafiki ni tatu; akizungumza anasema uongo… “

baadhi ya watu wamepewa mtihani na maradhi haya. Hajihisi raha na utulivu mpaka aseme uongo. Yeye siku zote tu husema uongo. Anakupiga stori kumbe ni uongo. Akikaa kwenye kikao anafanya vituko ili awachekeshe tu watu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ole wake yule anayesema uongo ili awachekeshe watu. Ole wake! Ole wake!”[1]

Amesema “Ola wake” mara tatu.

[1] Abu Daawuud (4990) na amesema kuwa ni Hasan

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/305)
  • Imechapishwa: 02/05/2023