Allaah (Ta´ala) amesema:

وَقَرْنَ فِي بُيُوتِكُنَّ وَلَا تَبَرَّجْنَ تَبَرُّجَ الْجَاهِلِيَّةِ الْأُولَىٰ

“Na tulizeni majumbani mwenu na wala msijishauwe mshauwo wa wanawake majahili wa awali.” (33:33)

Lililo bora kwa mwanamke ni asitoke nyumbani. Isipokuwa tu pale ambapo kutakuwa na dharurah ya kufanya hivo ni sawa. Atoke hali ya kuwa amejisitiri pasi na kujitia manukato wala kujipamba.

Vilevile ameamrisha mwanamke avae Hijaab mbele ya kila mwanaume asiyekuwa Mahram wake.

Hijaab ni ile ambayo mwanamke anafunika mwilipas wake mzima. Kiungo muhimu kuliko vyote ni uso. Ni wajibu kufunika uso mbele ya wanaume [wote] wasiokuwa Mahram zaidi kuliko ambavyo ni wajibu kufunika kichwa, mikono na kufunika miguu.

Maneno ya mwenye kusema kuwa inajuzu kuonyesha uso ni yenye kutupiliwa mbali. Maneno yake ni yenye kujigonga. Vipi itakuwa inajuzu kwa mwanamke kuonyesha uso wake na halafu iwe ni wajibu – kwa mujibu wake yeye – kufunika miguu yake? Ni kipi kilicho na fitina zaidi na kilicho karibu zaidi na zinaa: mwanamke kuonyesha miguu yake au uso wake? Jibu la kila mtu mwenye akili, ajuae alisemalo, atakuwa kusema lililo karibu zaidi na zinaa ni kuonyesha uso wake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/306-307)
  • Imechapishwa: 02/05/2023