07 – Sharti ya saba ya shaahadah – Mapenzi

Sharti ya saba ni kuipenda shahaadah na yale inayopelekea na kufahamishwa nayo na yale waliyowekewa katika Shari´ah wenye kuitamka, wenye kuitendea kazi, kushikamana na sharti zake na kuyachukia yanayoichengua. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَمِنَ النَّاسِ مَن يَتَّخِذُ مِن دُونِ اللّهِ

”Wapo katika watu ambao wanafanya badala ya Allaah washirika.”[1]

Allaah (´Azza wa Jall) akatueleza kuwa waja Wake waumini ni wenye kumpenda zaidi Yeye. Hilo ni kwa sababu hawakumshirikisha pamoja Naye yeyote katika kumpenda kama walivofanya wale washirikina wanaojidai kumpenda. Alama ya mja kumpenda Mola Wake ni yeye kutanguliza mbele yale anayoyapenda ijapo yatakuwa yanaenda kinyume na matamanio yake na kuyachukia yale yanayochukiwa na Mola Wake ijapo yatakuwa yanapendwa na matamanio yake. Aidha kunaingia pia kuwapenda wale wanaopendwa na Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kuwachukia wale wanaowachukia na pia kumfuata Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kumuigiliza na kukubali mwongozo wake.

Alama zote hizi ni sharti ya mapenzi. Haiwezekani kupatikana mapenzi ikiwa kutakosekana sharti hata moja. Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema:

أَرَأَيْتَ مَنِ اتَّخَذَ إِلَـٰهَهُ هَوَاهُ أَفَأَنتَ تَكُونُ عَلَيْهِ وَكِيلًا

“Je, umemuona yule aliyefanya matamanio yake kuwa ndio mungu wake? Je, hivi wewe utaweza kuwa ni mdhamini wake?”[2]

[1] 2:165

[2] 25:43

  • Muhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ma´aarij-ul-Qabuul (1/338)
  • Imechapishwa: 29/01/2025