Wanachinja kwenye makaburi kuomba mvua

Swali: Kuna ambao wanachinja kwenye makaburi kwa ajili ya mvua ambapo baadaye mvua inanyeha kwa muda wa siku mbili. Je, hiyo ni shirki?

Jibu: Huo ni mtihani na majaribio kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Kuhusu kuchinja kwenye makaburi ni shirki:

فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ

”Basi swali na uchinje kwa ajili ya Mola wako.”[1]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah amemlaani mwenye kuchinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah.”

Huo kama tulivosema ni mtihani. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:

وَلَنَبْلُوَنَّكُم بِشَيْءٍ مِّنَ الْخَوْفِ وَالْجُوعِ وَنَقْصٍ مِّنَ الْأَمْوَالِ وَالْأَنفُسِ وَالثَّمَرَاتِ ۗ وَبَشِّرِ الصَّابِرِينَ الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُم مُّصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا لِلَّـهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ أُولَـٰئِكَ عَلَيْهِمْ صَلَوَاتٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَرَحْمَةٌ ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُهْتَدُونَ

“Bila shaka Tutakujaribuni kwa kitu katika khofu na njaa na upungufu wa mali na nafsi na mazao [katika kazi zenu]. Wabashirie wale wenye kusubiri ambao unapowafika msiba basi husema: “Hakika sisi ni wa Allaah na hakika sisi Kwake ni wenye kurejea – hao zitakuwa juu yao baraka kutoka kwa Mola wao na rehema na hao ndio wenye kuongoka.”[2]

[1] 108:02

[2] 2:155-157

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 26-27
  • Imechapishwa: 28/01/2025