Yule ambaye amejizoweza kusimama usiku ndani ya Ramadhaan basi ahakikishe anaendelea kufanya kuswali kiasi anachoweza. Yule ambaye amejizoweza kufunga basi basi ahakikishe anaendelea kufunga kiasi anachoweza. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuhusu kusimama usiku katika Ramadhaan:

“Yeyote mwenye kusimama katika Ramadhaan kwa imani na kwa matarajio, basi atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia.”

Vivyo hivyo kuhusu swawm za kujitolea ambazo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema juu yake:

“Yule atakayefunga Ramadhaan kisha akaifuatishia [siku] sita za Shawwaal, basi anakuwa kama amefunga mwaka mzima.”[1]

Masiku sita haya ya Shawwaal ni mamoja yamefungwa mwanzoni mwa Shawwaal, katikati yake au mwishoni mwake, yote yamefungwa kwa kufuatanisha au kwa kuachanisha. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kufunga siku sita kila mwezi ni kama amefunga mwaka mzima.”

Ichunge afya yako kwa kufunga. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akifunga jumatatu na alkhamisi na akaulizwa juu ya hilo ambapo akasema:

“Matendo yanadhihirishwa jumatatu na alkhamisi. Napenda matendo yangu yadhihirishwe ilihali nimefunga.”

[1] al-Bukhaariy na Muslim.

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 10
  • Imechapishwa: 28/01/2025