Haafidhw Ibn Hajar al-´Asqalaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:
1 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Msiitangulizie Ramadhaan kwa kufunga siku moja au mbili. Isipokuwa mtu ambaye alikuwa akifunga swawm. Basi aiendeleze.”[1]
Hadiyth hii ni dalili ya makatazo ya kufunga kabla ya kuthibitishwa kuingia kwa mwezi wa Ramadhaan, kwa kufunga siku moja au mbili kwa lengo la kuchukua tahadhari ya Ramadhaan au kwa nia ya kujitolea. Katazo hili linapelekea hukumu ya uharamu kwa mujibu wa maoni yenye nguvu zaidi, kwa sababu huo msingi wake, isipokuwa pale ambapo kuna dalili inayoonyesha kinyume na hivo. Hadiyth kufanya mpaka wa siku moja au mbili ni kwa sababu hiyo ndiyo hiyo ndio mara nyingi kwa yule anayekusudia hivyo, lakini kufunga zaidi ya hapo kutajadiliwa baadaye.
Hata hivyo kuna baadhi ya hali ambazo zinabaguliwa kutokana na katazo hili. Nazo ni zifuatazo:
1 – Yule aliyekuwa na desturi ya kufunga siku fulani, kama jumatatu au alkhamisi, au kufunga siku moja na kufungua siku moja na hivyo ikatokea siku hiyo ikakutana na siku moja au mbili kabla ya kuanza Ramadhaan. Hii haina tatizo kwa kuwa sababu ya kutokuwepo katazo.
2 – Yule anayefunga swawm ya lazima, kama vile swamw ya nadhiri, kafara au kulipa deni la Ramadhaan iliyopita. Hili pia linafaa, kwa sababu hafanyi hivo kwa sababu ya kuikaribisha Ramadhaan.
Wanazuoni wamejadili hekima ya makatazo haya ambapo baadhi wakasema ni kwa ajili ya kutofautisha kati ya ´ibaadah za faradhi na za Sunnah. Sababu nyingine wametoa ni kujiandaa kwa ajili ya Ramadhaan kwa shauku na nguvu. Wengine wamesema ni kwa sababu hukumu ya kufunga imefungwa na kuonekana kwa mwezi mwandamo na hivyo kufunga kabla ya hapo ni kwenda kinyume na Shari´ah. Maoni haya ya pili ndio yamepewa nguvu na Haafidhw Ibn Hajar[2].
[1] al-Bukhaariy (1914) na Muslim (1082).
[2] Fat-ul-Baariy (4/168)).
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/7-8)
- Imechapishwa: 28/01/2025

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/7-8)
Imechapishwa: 28/01/2025
https://firqatunnajia.com/04-hadiyth-msiitangulizie-ramadhaan-kwa-kufunga-siku-moja-au-mbili/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)