Kwa mujibu wa dalili sahihi za Qur-aan na Sunnah kufunga Ramadhaan kumethibiti kuwa na fadhilah kubwa. Isitoshe kufunga kunapelekea thawabu kubwa na malipo makubwa sana kwa namna ya kwamba ikiwa nafsi iliyofunga ingeyatafakari, basi ingeruka kwa furaha na kutamani kwamba mwaka mzima uwe Ramadhaan. Kutokana na sababu hizi na nyenginezo ndio Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) akazifaradhishia nyumati zote kufunga. amesema (Ta´ala):
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ
“Enyi mlioamini! Mmeandikiwa [fardhi ya] swawm kama ilivyoandikwa kwa walio kabla yenu mpate kumcha Allaah.”[1]
Hata hivyo faida hizi hupatikana tu kwa yule anayefunga swawm kamili kwa namna ya kujiepusha na yale yote aliyoharamisha Allaah. Kwa msemo mwingine akajizuilia kutokamana na chakula, kinywaji na kujamiiana. Kadhalika akajizuilia na kusikiliza yaliyo haramu, kutazama yaliyo haramu, maneno ya haramu na machumo ya haramu. Isitoshe akahifadhi wakati wake na akafaidika na masiku ya mwezi katika kumtii Mola wake. Mtu sampuli hii ndiye ambaye anafaidika na swawm.
[1] 02:184
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/06)
- Imechapishwa: 28/01/2025
Kwa mujibu wa dalili sahihi za Qur-aan na Sunnah kufunga Ramadhaan kumethibiti kuwa na fadhilah kubwa. Isitoshe kufunga kunapelekea thawabu kubwa na malipo makubwa sana kwa namna ya kwamba ikiwa nafsi iliyofunga ingeyatafakari, basi ingeruka kwa furaha na kutamani kwamba mwaka mzima uwe Ramadhaan. Kutokana na sababu hizi na nyenginezo ndio Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) akazifaradhishia nyumati zote kufunga. amesema (Ta´ala):
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ
“Enyi mlioamini! Mmeandikiwa [fardhi ya] swawm kama ilivyoandikwa kwa walio kabla yenu mpate kumcha Allaah.”[1]
Hata hivyo faida hizi hupatikana tu kwa yule anayefunga swawm kamili kwa namna ya kujiepusha na yale yote aliyoharamisha Allaah. Kwa msemo mwingine akajizuilia kutokamana na chakula, kinywaji na kujamiiana. Kadhalika akajizuilia na kusikiliza yaliyo haramu, kutazama yaliyo haramu, maneno ya haramu na machumo ya haramu. Isitoshe akahifadhi wakati wake na akafaidika na masiku ya mwezi katika kumtii Mola wake. Mtu sampuli hii ndiye ambaye anafaidika na swawm.
[1] 02:184
Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/06)
Imechapishwa: 28/01/2025
https://firqatunnajia.com/03-mtu-ambaye-anafaidika-na-swawm/