Swawm inayo faida nyingi na hukumu nyingi ambapo miongoni mwazo ni:

1 – Kufunga ni moja ya msaada mkubwa wa kumcha Allaah, kwa sababu ina athari ya ajabu katika kuhifadhi viungo vya nje na nguvu za ndani.

2 – Kumuabudu Allaah (Ta´ala) kwa kuacha matamanio ya nafsi na yale mambo iliyozowea, jambo ambalo linaonyesha ukweli wa mapenzi ya mja kwa Mola wake na kumtukuza na kutafuta radhi Zake. Ametanguliza mbele yale anayoyapenda na kuyaridhia Allaah mbele ya kile kinachotamaniwa na nafsi na matamanio yake.

3 – Kufunga ni malezi ya kudhibiti matakwa, kupambana na nafsi na kuizoweza subira na uvumilivu kwa yale yanayoipelekea manufaa.

4 – Kufunga kuna faida kubwa za kiafya; husafisha mwili kutokana na mchanganyo mbaya wa chakula na kumpa mtu afya na nguvu kwa kupanga nyakati za kula na kuupumzisha mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kwa muda fulani, kama walivyothibitisha madaktari bingwa waliotibu wagonjwa wao kwa kufunga.

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/06)
  • Imechapishwa: 28/01/2025