27 – ´Abd [tupu] bin Munkadir ametuhadithia: al-Mughiyrah bin ´Abdillaah ametuhadithia, kutoka kwa ´Aaswim bin Muhammad al-´Umariy, kutoka kwa baba yake, aliyesema:

”´Umar bin al-Khattwaab alikuwa akitoa vimelea kutoka kwenye kwato za ngamia wa swadaqah. Siku moja akaja nyumbani baada ya kupigwa na jua akasema: ”Mna chochote?” Mke wake akasema: ”Chini ya kitanda.” Akachukua sahani iliokuwa na tende akala. Kisha akanywa maji. Baada ya hapo akafuta tumbo lake na kusema: ”Ole wake ambaye tumbo lake litamwingiza Motoni!”

28 – Hishaam bin al-Haarith ametuhadithia: ´Ubaydullaah bin ´Amr ametuhadithia, kutoka kwa ´Abdul-Malik bin ´Umayr, kutoka kwa ´Abdur-Rahmaan bin Abiy Bakrah, kutoka kwa baba yake, ambaye ameeleza:

”´Umar bin al-Khattwaab aliletewa mkate na mafuta, ambapo akawa anazila na kufuta tumbo lake na kusema: ”Naapa kwa Allaah! Utazowea tu, ee tumbo, mkate na mafuta, muda wa kuwa siagi inauzwa kwenye vikapu.”

29 – ´Ubayd bin Muhammad amenihadithia: Ibraahiym bin Bukayr ametuhadithia: Twalhah bin Zayd al-Qurashiy ametuhadithia, kutoka kwa [tupu] al-Bakhtariy, ambaye amesimulia kuwa ´Umar bin al-Khattwaab aliwaambia marafiki zake:

”Kama sikuchelea kurefushiwa hesabu kesho, basi ningeamrisha mwanakondoo akachomwa kwenye oveni.”

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Juu´, uk. 45-46
  • Imechapishwa: 11/06/2023