Unachotakiwa ni wewe kuamini kuwepo kwa Allaah, uola Wake, kuabudiwa na majina na sifa Zake. Ni lazima kwa mtu kuamini haya.

Yule mwenye kupinga kuwepo kwa Allaah ni kafiri na atadumishwa Motoni milele. Yule mwenye kutilia shaka kuwepo kwa Allaah ni kafiri. Ni lazima kuamini kabisa ya kwamba Allaah yuhai, Mjuzi, Muweza na Yupo. Yule mwenye kutilia shaka uola Wake ni kafiri.

Yule mwenye kumshirikisha pamoja Naye yeyote katika uola wake ni kafiri. Kwa mfano mwenye kusema kuwa mawalii wanaendesha ulimwengu, wana taathira katika ulimwengu, hivyo akawaomba, akataka uokozi na nusura kutoka kwao, huyu ni kafiri. Kwa kuwa hakumuamini Allaah.

Yule mwenye kufanya kitu katika mambo ya ´ibaadah akamfanyia asiyekuwa Allaah ni kafiri. Hakuamini upwekekaji katika ‘ibaadah. Mwenye kusujudia jua, mwezi, mti, mto, bahari, mlima, Malaika, Mtume yeyote, walii yeyote, ni kafiri. Kufuru yake ni yenye kumtoa katika Uislamu kwa kuwa amemshirikisha Allaah pamoja Naye mwingine.

Vilevile mwenye kupinga, kwa njia ya kukadhibisha, kitu miongoni mwa yale Aliyojisifia Yeye Mwenyewe, ni kafiri. Kwa kuwa amemkadhibisha Allaah na Mtume Wake. Akipinga sifa miongoni mwa sifa za Allaah, kwa njia ya ukadhibishaji, huyu ni kafiri kwa kukadhibisha kwake yaliyokuja katika Qur-aan na Sunnah. Kwa mfano akisema kuwa Allaah hakulingana juu ya ´Arshi na wala hashuki katika mbingu ya dunia, huyu ni kafiri. Lakini ikiwa atakipingakwa njia ya kukifasiri kimakosa,kutaangaliwa kama ufasiri wake ni wenye nafasi yenye kukubalika katika Ijtihaad au hapana. Ikiwa ufasiri wake una nafasi ya kutazamwa, hafanyiwi Takfiyr bali atafanyiwa Tafsiyq kwa kuwa ametoka katika mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Ama ikiwa ufasiri wake hauna nafasiya kutazamwa, jambo hili ni kama upingaji wa kukadhibisha. Huyu pia anakuwa kafiri.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/433-434)
  • Imechapishwa: 11/06/2023