Kufunga Ramadhaan ni nguzo miongoni mwa nguzo za Uislamu ambayo Uislamu hautimii isipokuwa kwayo. Lakini hata hivyo sio wajibu isipokuwa kwa yule aliyetimiza sharti zifuatazo:

1 – Muislamu.

2 – Aliyebaleghe.

3 – Aliye na akili.

4 – Muweza.

5 – Mkazi.

6 – Asiye na kizuizi.

Ikiwa ni mdogo swawm haimuwajibikii. Ikiwa ni mwendawazimu swawm haimuwajibikii. Ikiwa ni kafiri swawm haimuwajibikii. Kuhusu mtu ambaye si muweza wamegawanyika sehemu mbili:

1 – Ikiwa si muweza ambaye kunatarajiwa kizuizi chake kuondoka,  kwa mfano mtu mwenye maradhi ambayo yataisha, atakula kisha atalipa siku zake kutegemea na siku alizokula.

2 – Ikiwa si muweza ambaye hakutarajiwi kizuizi chake kuondoka, kwa mfano mtu mzee sana, atalisha kwa kila siku moja masikini. Ikiwa ni mkazi kinyume chake ni msafiri. Msafiri hana juu yake swawm lakini hata hivyo anatakiwa kulipa siku zingine.

Asiyekuwa na kizuizi ni kama mtu mwenye hedhi na nifasi. Watu hawa wawili swawm haiwawajibikii. Bali haijuzu kwao kufunga. Lakini hata hivyo wanatakiwa kulipa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/429-430)
  • Imechapishwa: 11/06/2023