23 – al-Husayn bin al-Junayd ametuhadithia: Ghassaan bin ´Ubayd al-Azdiy al-Mawsiliy ametuhadithia: Hamzah al-Baswriy ametuhadithia, kutoka kwa Hishaam bin ´Urwah, kutoka kwa baba yake, ambaye amesimulia kuwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:

”Hakika janga la kwanza lililoupata ummah huu, baada ya kufariki Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ni shibe. Pindi watu wanaposhiba matumbo yao, miili yao inakuwa mikubwa, mioyo yao inakuwa migumu na matamanio yao hayazuiliki.”

23 – Ahmad bin ´Uthmaan al-Awdiy ametuhadithia: Qaasim bin Qays an-Nakha´iy ametuhadithia: Humayd bin al-Muthannaa ametuhadithia, kutoka kwa Abu Ja´far, ambaye amesema:

”Wakati tumbo linapojaa, mwili huzidi kupitiliza.”

24 – ´Abdur-Rahmaan bin Swaalih ametuhadithia: Yuunus bin Bukayr ametuhadithia, kutoka kwa ´Anbasah bin al-Azhar, kutoka kwa Yahyaa bin ´Aqiyl, ambaye ameeleza kuwa ´Aliy bin Abiy Twaalib alimwambia ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anhumaa):

”Kama unataka kuungana na marafiki zako wawili, basi fupisha matumaini, kula bila kushiba, punguza kanzu yako, vaa kikoi chako nje ndani na tengeneza viatu – hapo utaungana nao.”

25 – Ahmad bin ´Iysaa ametuhadithia: ´Abdullaah bin Wahb ametuhadithia: Sa´iyd bin Abiy Ayyuub amenihadithia, kutoka kwa Abu Khallaad, kutoka kwa ´Ubaadah bin as-Swaamit, ambaye alikuwa akisema:

”Tumbo hutaka tena na tena. Yanakutoshelezeni yale yenye kutosheleza.”

26 – Ahmad bin ´Iysaa ametuhadithia: ´Abdullaah bin Wahb ametuhadithia, kutoka kwa Khaalid bin Humayd, kutoka kwa ´Abdullaah bin al-Haarith, kutoka kwa Qays bin Raafiy´, aliyesema:

”Ole wake ambaye tumbo lake ndio dini yake, dunia hamu yake.”

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Juu´, uk. 43-45
  • Imechapishwa: 11/06/2023