389 – Abu Faatwimah (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Nilisema: “Ee Mtume wa Allaah! Nieleze kuhusu kitendo ambacho nitanyooka juu yake na kukifanya.” Akasema:

عليكَ بالسجودِ، فإنَّك لا تسجدُ لله سجدَةً، إلا رَفَعَكَ اللهُ بها درجةً، وحَطَّ عنك بها خَطيئةً

“Lazimiana na Sujuud. Kwani hakika hutomsujudia Allaah sijda, isipokuwa atakunyanyua kwayo ngazi na kukufutia kwayo kosa.”[1]

Ameipokea Ibn Maajah kwa cheni ya wapokezi nzuri.

Ahmad ameipokea kwa kifupi kwa tamko lisemalo:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alinambia:

يا أبا فاطمة إنْ أردتَ أنْ تلقاني فأكثرِ السجودَ

“Ee Abu Faatwimah! Kama unataka kukutana nami, basi hakikisha unasujudu kwa wingi.”[2]

[1] Nzuri na Swahiyh.

[2] Nzuri kupitia zingine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/279)
  • Imechapishwa: 28/11/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy