06. ´Aqiydah sahihi juu ya Mitume ya Allaah

Kuhusu imani ya kuwaamini Mitume, inatakiwa iwe kwa usadikishaji wa kukata kabisa ya kwamba Allaah ameutumia kila Ummah Mtume ambaye aliwalingania katika kumuabudu Allaah pekee na kukufuru vile vyote vinavyoabudiwa badala Yake.

Katika hili kunaingia pia ya kwamba wote ni wakweli, wenye kusadikishwa, wema, waongofu, wachaji Allaah, waaminifu na waongofu na wenye kuongoza. Wote wamefikisha ujumbe wa Allaah.

Allaah alimfanya Ibraahiym kuwa kipenzi wa hali ya juu na kadhalika akamfanya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwa kipenzi wa hali ya juu. Allaah alimzungumzisha Muusa maneno ya kweli na akamnyanyua Idriys nafasi ya juu. ´Iysaa ni mja na Mtume wa Allaah, ni neno Lake tu alilompelekea Maryam na ni roho iliyotoka Kwake.

Allaah amewafadhilisha baadhi juu ya wengine na akawanyanyua daraja baadhi juu ya wengine.

Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndio bwana wa wanadamu siku ya Qiyaamah na ni jambo litapitika pasi na ufakhari.

Ulinganizi wa Mitume wote ulikuwa ni wenye kuafikiana katika msingi wa dini, nako ni kumpwekesha Allaah (Ta´ala) katika ´ibaadah Yake, uola Wake na majina na sifa Zake. Amesema (Ta´ala):

إِنَّ الدِّينَ عِندَ اللَّـهِ الْإِسْلَامُ

“Hakika dini mbele ya Allaah ni Uislamu.” (03:19)

وَمَن يَبْتَغِ غَيْرَ الْإِسْلَامِ دِينًا فَلَن يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ

“Na yeyote anayetaka dini isiyokuwa ya Kiislamu basi haitokubaliwa kwake naye Aakhirah atakuwa miongoni mwa waliokhasirika.” (03:19)

Amesema (Ta´ala) kuhusu Nuuh:

وَأُمِرْتُ أَنْ أَكُونَ مِنَ الْمُسْلِمِينَ

“Na nimeamrishwa niwe miongoni mwa waislamu.” (10:72)

Kadhalika amesema (Ta´ala) kuhusu Muusa:

وَقَالَ مُوسَىٰ يَا قَوْمِ إِن كُنتُمْ آمَنتُم بِاللَّـهِ فَعَلَيْهِ تَوَكَّلُوا إِن كُنتُم مُّسْلِمِينَ

“Enyi watu wangu! Ikiwa mmemwamini Allaah, basi Kwake mtegemee, mkiwa ni waislamu.” (10:84)

Vivyo hivyo amesema (Ta´ala) kuhusu Sulaymaan pindi Balqiys aliposema:

رَبِّ إِنِّي ظَلَمْتُ نَفْسِي وَأَسْلَمْتُ مَعَ سُلَيْمَانَ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ

“Mola wangu! Hakika mimi nimejidhulumu nafsi yangu! Na hivi sasa nimesilimu pamoja na Sulaymaan kwa Allaah, Mola wa walimwengu!” (27:44)

Amesema (Ta´ala):

شَرَعَ لَكُم مِّنَ الدِّينِ مَا وَصَّىٰ بِهِ نُوحًا وَالَّذِي أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ وَمَا وَصَّيْنَا بِهِ إِبْرَاهِيمَ وَمُوسَىٰ وَعِيسَىٰ ۖ أَنْ أَقِيمُوا الدِّينَ وَلَا تَتَفَرَّقُوا فِيهِ ۚ كَبُرَ عَلَى الْمُشْرِكِينَ مَا تَدْعُوهُمْ إِلَيْهِ ۚ اللَّـهُ يَجْتَبِي إِلَيْهِ مَن يَشَاءُ وَيَهْدِي إِلَيْهِ مَن يُنِيبُ

“Amekuwekeeni Shari´ah katika dini yale aliyomuusia kwayo Nuuh, na ambayo tumekufunulia Wahy na tuliyomuusia kwayo Ibraahiym na Muusa na ‘Iysaa kwamba simamisheni dini na wala msifarikiane humo. Yamekuwa makubwa kwa washirikina yale unayowalingania. Allaah anamteua Kwake amtakaye na anamwongoza Kwake anayerudiarudia .” (42:13)

Mitume walikuwa 315 na Manabii 124.000. Haya yamethibiti katika Hadiyth kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutoka katika Hadiyth ya Abu Umaamah na ya Abu Dharr[1].

Tofauti kati ya Mtume na Nabii, ni kwamba Nabii ni yule ambaye anapokea Wahy kutoka kwa Allaah. Akitumilizwa vilevile kwa wale wenye kwenda kinyume na maamrisho ya Allaah ili afikishe ujumbe wa Allaah, anahesabika kuwa Mtume. Ama yule ambaye anatendea kazi Shari´ah ya kabla yake na asitumilizwe kwa yeyote ili kufikisha ujumbe kutoka kwa Allaah, anahesabika kuwa Nabii na sio Mtume[2]. Mujaahid (Rahimahu Allaah) amesema:

“Nabii ni yule anayezungumzishwa na kuteremshiwa Wahy kutoka kwa Allaah na wala hatumilizwi [kwa watu].”

Kujengea juu ya haya ni kwamba kila Mtume ni Nabii na sio kila Nabii anakuwa Mtume.

Allaah (Ta´ala) ametaja wengi katika wao. Kwa mfano Aadam, Nuuh, Idriys, Huud, Swaalih, Ibraahiym, Ismaa´iyl, Ishaaq, Ya´quub, Yuusuf, Luutw, Shu´ayb, Yuunus, Muusa, Haaruun, Ilyaas, Zakariyyah, Yahyaa, al-Yasaa´, Dhul-Kifl, Daawuud, Sulaymaan, Ayyuub, asbaatw (vizazi), ´Iysaa na Muhammad – Swalah na salamu ziwaendee wote. Allaah ametueleza khabari zao ambazo ndani yake mna mafunzo, mazingatio na mawaidha:

وَرُسُلًا قَدْ قَصَصْنَاهُمْ عَلَيْكَ مِن قَبْلُ وَرُسُلًا لَّمْ نَقْصُصْهُمْ عَلَيْكَ ۚ وَكَلَّمَ اللَّـهُ مُوسَىٰ تَكْلِيمًا

“Na Mitume Tuliokwishakusimulia habari zao kabla na Mitume [wengine ambao] hatukukusimulia habari zao – na bila shaka Allaah alimzungumzisha Muusa maneno ya kikweli.” (04:164)

Kwa hivyo tunawaamini wote kwa ufafanuzi pale wanapotajwa kwa ufafanuzi na kwa jumla pale wanapotajwa kwa jumla.

Tunaamini kuwa Mitume na Manabii wote ni wanadamu walioumbwa na hawana sifa yoyote ile ya kiungu. Amesema (Ta´ala):

قُلْ إِنَّمَا أَنَا بَشَرٌ مِّثْلُكُمْ يُوحَىٰ إِلَيَّ أَنَّمَا إِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۖ فَمَن كَانَ يَرْجُو لِقَاءَ رَبِّهِ فَلْيَعْمَلْ عَمَلًا صَالِحًا وَلَا يُشْرِكْ بِعِبَادَةِ رَبِّهِ أَحَدًا

“Sema: “Hakika mimi ni mtu kama nyinyi isipokuwa tu nafunuliwa Wahy kwamba: “Hakika mungu wenu wa haki ni mungu Mmoja pekee. Hivyo basi anayetaraji kukutana na Mola wake na atende matendo mema na wala asishirikishe katika ‘ibaadah za Mola wake yeyote.” (18:110)

قَالَتْ لَهُمْ رُسُلُهُمْ إِن نَّحْنُ إِلَّا بَشَرٌ مِّثْلُكُمْ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَمُنُّ عَلَىٰ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ ۖ وَمَا كَانَ لَنَا أَن نَّأْتِيَكُم بِسُلْطَانٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ ۚ وَعَلَى اللَّـهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ

“Mitume wao wakawaambia: “Sisi si chochote isipokuwa ni watu kama nyinyi, lakini Allaah anamfadhilisha amtakaye miongoni mwa waja Wake. Na haikutupasa sisi kukujieni kwa hoja mnazotaka isipokuwa kwa idhini ya Allaah – na kwa Allaah pekee wanategemea waumini.” (14:11)

وَمَا أَرْسَلْنَا قَبْلَكَ مِنَ الْمُرْسَلِينَ إِلَّا إِنَّهُمْ لَيَأْكُلُونَ الطَّعَامَ وَيَمْشُونَ فِي الْأَسْوَاقِ ۗ وَجَعَلْنَا بَعْضَكُمْ لِبَعْضٍ فِتْنَةً أَتَصْبِرُونَ ۗ وَكَانَ رَبُّكَ بَصِيرًا

“Na Hatukupeleka kabla yako Mitume wowote isipokuwa bila shaka walikuwa wanakula chakula na wanatembea masokoni. Na tumejaalia baadhi yenu nyinyi kwa nyinyi kuwa ni majaribio je mtavumilia? Na Mola wako daima ni Mwenye kuona!” (25:20)

قُل لَّا أَقُولُ لَكُمْ عِندِي خَزَائِنُ اللَّـهِ وَلَا أَعْلَمُ الْغَيْبَ وَلَا أَقُولُ لَكُمْ إِنِّي مَلَكٌ ۖ إِنْ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰ إِلَيَّ ۚ قُلْ هَلْ يَسْتَوِي الْأَعْمَىٰ وَالْبَصِيرُ ۚ أَفَلَا تَتَفَكَّرُونَ

“Sema: “Sikuambieni kuwa mimi nina hazina ya Allaah na wala kwamba najua ya ghaibu na wala sikuambieni kuwa mimi ni Malaika. Sifuati isipokuwa yale nilofunuliwa Wahy“. Sema: “Je, analingana sawasawa kipofu na mwenye kuona – basi hamtafakari?” (06:50)

قُل لَّا أَمْلِكُ لِنَفْسِي نَفْعًا وَلَا ضَرًّا إِلَّا مَا شَاءَ اللَّـهُ ۚ وَلَوْ كُنتُ أَعْلَمُ الْغَيْبَ لَاسْتَكْثَرْتُ مِنَ الْخَيْرِ وَمَا مَسَّنِيَ السُّوءُ ۚ إِنْ أَنَا إِلَّا نَذِيرٌ وَبَشِيرٌ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ

“Sema: “Siimilikii nafsi yangu manufaa yoyote wala dhara yoyote isipokuwa atakavyo Allaah na lau ningekuwa najua ya ghaibu, bila shaka ningelijikithirishia ya kheri na wala lisingelinigusa ovu. Mimi si chochote isipokuwa ni mwonyaji na mbashiriaji kwa watu wanaoamini.” (07:188)

Tunaamini kuwa ni waja miongoni mwa waja wa Allaah ambao Allaah amewaheshimisha kwa Ujumbe. Amewasifu kuwa ni waja pindi zinapotajwa nafasi zao kuu na pindi anapowasifu.

Tunaamini kuwa Allaah (Ta´ala) amekhitimisha nyujumbe kwa Ujumbe wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kwamba alimtuma kwa walimwengu wote majina na  watu:

قُلْ يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنِّي رَسُولُ اللَّـهِ إِلَيْكُمْ جَمِيعًا

“Sema: “Enyi  watu! Hakika mimi ni Mtume wa Allaah kwenu nyinyi nyote.” (07:158)

وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا رَحْمَةً لِّلْعَالَمِينَ

“Na Hatukukutuma isipokuwa uwe ni rehema kwa walimwengu.” (21:107)

وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا كَافَّةً لِّلنَّاسِ بَشِيرًا وَنَذِيرًا وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ

“Na Hatukukutuma isipokuwa kwa watu wote hali ya kuwa ni mbashiriaji na muonyaji, lakini watu wengi hawajui.” (34:28)

Ameeleza (Ta´ala) kuwa amechukua ahadi kwa Mitume endapo wataishi zama za Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) basi wamfuate. Hapa kuna dalili ya wazi kabisa ya kwamba Ujumbe wake ndio wa mwisho na kuwa unafuta nyujumbe zingine zote zilizotangulia. Amesema (Ta´ala):

وَإِذْ أَخَذَ اللَّـهُ مِيثَاقَ النَّبِيِّينَ لَمَا آتَيْتُكُم مِّن كِتَابٍ وَحِكْمَةٍ ثُمَّ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مُّصَدِّقٌ لِّمَا مَعَكُمْ لَتُؤْمِنُنَّ بِهِ وَلَتَنصُرُنَّهُ ۚ قَالَ أَأَقْرَرْتُمْ وَأَخَذْتُمْ عَلَىٰ ذَٰلِكُمْ إِصْرِي ۖ قَالُوا أَقْرَرْنَا ۚ قَالَ فَاشْهَدُوا وَأَنَا مَعَكُم مِّنَ الشَّاهِدِينَ فَمَن تَوَلَّىٰ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ

“Na pale Allaah alipochukua ahadi kwa Manabii: “Nikisha kupeni Kitabu na  hekima, kisha akakujieni Mtume mwenye kusadikisha mliyo nayo, ni juu yenu mumuamini na  mumnusuru.” Akasema: “Je, mmekiri nammekubali kushika agizo langu juu ya hayo?” Wakasema: “Tumekubali.” Akasema: “Basi shuhudieni na Mimi nipamoja nanyi katika kushuhudia. Watakaogeuka baada ya haya basi hao ndio mafusaki.” (03:81-82)

Mitume walikuja na bishara njema juu ya Ujumbe wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) – swalah na salamu ziwe juu yao wote. Amesema (Ta´ala):

وَإِذْ قَالَ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ إِنِّي رَسُولُ اللَّـهِ إِلَيْكُم مُّصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيَّ مِنَ التَّوْرَاةِ وَمُبَشِّرًا بِرَسُولٍ يَأْتِي مِن بَعْدِي اسْمُهُ أَحْمَدُ ۖ فَلَمَّا جَاءَهُم بِالْبَيِّنَاتِ قَالُوا هَـٰذَا سِحْرٌ مُّبِينٌ

“Na kumbuka wakati ´Iysaa mwana wa Maryam aliposema: “Enyi wana wa Israaiyl! Hakika mimi ni Mtume wa Allaah kwenu mwenye kusadikisha yaliyo kabla yangu katika Tawraat na mwenye kubashiria kuja kwa Mtume baada yangu jina lake Ahmad.” Basi alipowajia kwa hoja za wazi, walisema: “Huu ni uchawi wa wazi.” (61:06)

وَاكْتُبْ لَنَا فِي هَـٰذِهِ الدُّنْيَا حَسَنَةً وَفِي الْآخِرَةِ إِنَّا هُدْنَا إِلَيْكَ ۚ قَالَ عَذَابِي أُصِيبُ بِهِ مَنْ أَشَاءُ ۖ وَرَحْمَتِي وَسِعَتْ كُلَّ شَيْءٍ ۚ فَسَأَكْتُبُهَا لِلَّذِينَ يَتَّقُونَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَالَّذِينَ هُم بِآيَاتِنَا يُؤْمِنُونَ الَّذِينَ يَتَّبِعُونَ الرَّسُولَ النَّبِيَّ الْأُمِّيَّ الَّذِي يَجِدُونَهُ مَكْتُوبًا عِندَهُمْ فِي التَّوْرَاةِ وَالْإِنجِيلِ

“Na Tuandikie katika dunia hii mazuri na katika Aakhirah. Hakika sisi tumerudi kutubu Kwako.” Akasema: “Adhabu Yangu nitamsibu nayo nimtakaye na rehema Yangu imekienea kila kitu. Basi nitawahukumia wale wenye kumcha Allaah na wanaotoa zakaah na ambao wao wanaziamini Aayah Zetu. Wale wanomfuata Mtume, Nabii asiyejua kuandika na kusoma, wanamkuta ameandikwa kwao katika Tawraat na Injiyl.” (07:156-157)

Katika “as-Swahiyh” ya Muslim imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Naapa kwa yule ambaye nafsi ya Muhammad iko mikononi Mwake. Hatosikia kuhusu mimi sawa awe myahudi au mkristo kisha akafa na asiamini yale niliyotumwa kwayo isipokuwa atakuwa katika watu wa Motoni.”

Yule mwenye kukanusha Ujumbe wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa walimwengu wote, amewakanusha Mitume wote hata yule Mtume ambaye anadai kuwa anamuamini na kumfuata. Amesema (Ta´ala):

كَذَّبَتْ قَوْمُ نُوحٍ الْمُرْسَلِينَ

“Watu wa Nuuh walikadhibisha Mitume.” (26:105)

Amefanya kuwa waliwakadhibisha Mitume wote pamoja na kuwa Nuuh ndiye alikuwa Mtume wa kwanza.

Tunaamini kuwa hakuna Nabii yoyote baada ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Yule mwenye kudai kuwa kuna Nabii mwingine baada yake, amekufuru. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَلَـٰكِن رَّسُولَ اللَّـهِ وَخَاتَمَ النَّبِيِّينَ

“Lakini ni Mtume wa Allaah na ni mwisho wa Manabii.” (33:40)

Katika “as-Swahiyh” ya Muslim imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Nimefadhilishwa juu ya Mitume wengine kwa mambo sita: nimepewa maneno ambayo ni machache lakini yenye maana pana, nimenusuriwa kwa woga [unaotiwa kwenye nyoyo za maadui], nimehalalishiwa mateka, nimefanyiziwa ardhi yote kuwa mahali pa kuswalia tena safi, nimetumwa kwa viumbe wote na mimi ndiye Nabii wa mwisho.”

Mwenye kukanusha Ujumbe wa Nabii au Mtume yoyote, amekufuru kwa maafikiano ya waislamu. Amesema (Ta´ala):

إِنَّ الَّذِينَ يَكْفُرُونَ بِاللَّـهِ وَرُسُلِهِ وَيُرِيدُونَ أَن يُفَرِّقُوا بَيْنَ اللَّـهِ وَرُسُلِهِ وَيَقُولُونَ نُؤْمِنُ بِبَعْضٍ وَنَكْفُرُ بِبَعْضٍ وَيُرِيدُونَ أَن يَتَّخِذُوا بَيْنَ ذَٰلِكَ سَبِيلًا أُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ حَقًّا ۚ وَأَعْتَدْنَا لِلْكَافِرِينَ عَذَابًا مُّهِينًا وَالَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّـهِ وَرُسُلِهِ وَلَمْ يُفَرِّقُوا بَيْنَ أَحَدٍ مِّنْهُمْ أُولَـٰئِكَ سَوْفَ يُؤْتِيهِمْ أُجُورَهُمْ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا

“Hakika wale waliomkufuru Allaah na Mitume Wake na wanataka kufarikisha kati ya Allaah na Mitume Wake na wanasema: “Tunaamini baadhi [ya Mitume] na tunawakanusha wengine” na wanataka kuchukua njia iliyo baina ya hayo – hakika hao ndio makafiri wa kweli na tumewaandalia makafiri adhabu ya kutweza. Na wale waliomwamini Allaah na Mitume Yake na hawakufarikisha yeyote kati yao,basi  hao atawapa ujira wao na Allaah daima ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.” (04:150-152)

[1] Tazama ”Silsilah al-Ahaadiyth as-Sahiyhah” (6/358/2668) ya Imam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy.

[2] ”an-Nubuwwaat” ya Shaykh-ul-Islaam, uk. 255.

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Mu´taqad as-Swahiyh, uk. 44-50
  • Imechapishwa: 21/06/2020