Swali: Unawanasihi nini Salafiyyuun Oman wanaoishi kati ya Khawaarij na mapote mengine? Ni vipi mtu atatangamana na mapote na makundi hayo?

Jibu: Lililo la wajibu kwa mja ni yeye kumcha Allaah kiasi na anavyoweza na atekeleze yale aliyomwamrisha Allaah kiasi na anavyoweza. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

”Mcheni Allaah muwezavyo.”[1]

Akilazimika kuwa na mawasiliano na mapote, basi afanye biashara nao pasi na kujiachia, kuzungumza nao, kufanya nao matani wala chochote katika hayo. Haya ndio yanayomlazimu kutokana na vile ninavyoona.

[1] 64:16

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fath-ur-Rahiym al-Waduud, uk. 253
  • Imechapishwa: 21/06/2020