07. ´Aqiydah sahihi juu ya siku ya Mwisho

Kuhusu kuamini siku ya Mwisho, ni siku ya Qiyaamah na yale mambo na hali zitazopitika ndani yake. Ahl-us-Sunnah wanaamini hilo kwa yakini. Amesema (Ta´ala):

وَبِالْآخِرَةِ هُمْ يُوقِنُونَ

“Na ni wenye yakini juu ya Aakhirah.” (02:04)

اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۚ لَيَجْمَعَنَّكُمْ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ لَا رَيْبَ فِيهِ ۗ وَمَنْ أَصْدَقُ مِنَ اللَّـهِ حَدِيثًا

“Allaah, hakuna mungu wa haki isipokuwa Yeye – bila ya shaka atakukusanyeni siku ya Qiyaamah haina shaka ndani yake. Na nani mkweli zaidi katika maneno kuliko Allaah?” (04:87)

وَإِنَّ السَّاعَةَ لَآتِيَةٌ

“Hakika Saa bila shaka itafika.” (15:85)

Katika hilo kunaingia vilevile kuamini Ufufuliwaji, nayo ni ile Siku maiti watahuishwa. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَنُفِخَ فِي الصُّورِ فَصَعِقَ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَمَن فِي الْأَرْضِ إِلَّا مَن شَاءَ اللَّـهُ ۖ ثُمَّ نُفِخَ فِيهِ أُخْرَىٰ فَإِذَا هُمْ قِيَامٌ يَنظُرُونَ

“Na itapulizwa katika baragumu watazimia wale walioko mbinguni na ardhini isipokua amtakaye Allaah. Kisha litapulizwa humo jengine tahamaki hao wanasimama wakitazama.” (39:68)

كَمَا بَدَأْنَا أَوَّلَ خَلْقٍ نُّعِيدُهُ ۚ وَعْدًا عَلَيْنَا ۚ إِنَّا كُنَّا فَاعِلِينَ

“Kama Tulivyoanza uumbaji umbo la mwanzo tutalirudisha. Hiyo ni ahadi juu Yetu – hakika sisi ni wafanyao.” (21:104)

Katika haya kunaingia pia kuamini madaftari ya matendo ambayo yatagawanywa kwa mkono wa kulia au wa kushoto nyuma ya mgongo. Allaah (Ta´ala) amesema:

فَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ بِيَمِينِهِ فَيَقُولُ هَاؤُمُ اقْرَءُوا كِتَابِيَهْ إِنِّي ظَنَنتُ أَنِّي مُلَاقٍ حِسَابِيَهْ فَهُوَ فِي عِيشَةٍ رَّاضِيَةٍ فِي جَنَّةٍ عَالِيَةٍ قُطُوفُهَا دَانِيَةٌ كُلُوا وَاشْرَبُوا هَنِيئًا بِمَا أَسْلَفْتُمْ فِي الْأَيَّامِ الْخَالِيَةِ وَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ بِشِمَالِهِ فَيَقُولُ يَا لَيْتَنِي لَمْ أُوتَ كِتَابِيَهْ وَلَمْ أَدْرِ مَا حِسَابِيَهْ يَا لَيْتَهَا كَانَتِ الْقَاضِيَةَ مَا أَغْنَىٰ عَنِّي مَالِيَهْ ۜ هَلَكَ عَنِّي سُلْطَانِيَهْ خُذُوهُ فَغُلُّوهُ ثُمَّ الْجَحِيمَ صَلُّوهُ ثُمَّ فِي سِلْسِلَةٍ ذَرْعُهَا سَبْعُونَ ذِرَاعًا فَاسْلُكُوهُ إِنَّهُ كَانَ لَا يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ الْعَظِيمِ وَلَا يَحُضُّ عَلَىٰ طَعَامِ الْمِسْكِينِ فَلَيْسَ لَهُ الْيَوْمَ هَاهُنَا حَمِيمٌ وَلَا طَعَامٌ إِلَّا مِنْ غِسْلِينٍ لَّا يَأْكُلُهُ إِلَّا الْخَاطِئُونَ

“Ama yule atakayepewa kitabu chake kuliani mwake, atasema: “Hebu chukueni someni kitabu changu! Hakika mimi niliyakinisha kuwa hakiki mimi ni mwenye kukutana na hesabu yangu!” Basi yeye atakuwa katika maisha ya kuridhisha. Kwenye Pepo ya juu. Matunda yake ya kuchumwa ni karibu. [Wataambiwa]: “Kuleni na kunyweni kwa furaha kwa yale mliyoyatanguliza katika siku nyingi zilopita!” Na ama yule atakayepewa kitabu chake kushotoni mwake, atasema: “Ee, laiti nisingelipewa kitabu changu na wala nisingelijua hesabu yangu! Ee, laiti yangelikuwa mauti ndio kumalizika kwangu! Haikunifaa mali yangu! Ufalme wangu umeangamia!” [Kutasemwa]: “Mchukueni na mfungeni pingu kisha kwenye [Moto wa] al-Jahiym mwingizeni aungue. Halafu katika minyororo yenye urefu wa dhiraa sabini mtieni pingu. Hakika yeye alikuwa hamuamini Allaah Mkuu na wala hahamasishi kulisha masikini. Basi leo hapa hatokuwa na rafiki wa dhati, na wala [hawatopata] chakula isipokuwa maji ya vidonda vilooshwa [vya walio Motoni]. Hawakili [chakula] hicho isipokuwa wenye hatia.” (69:19-37)

Vilevile kuamini Mizani itayowekwa siku ya Qiyaamah na hivyo hakuna yoyote atayedhulumiwa kitu. Amesema (Ta´ala):

فَمَن ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ وَمَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ فِي جَهَنَّمَ خَالِدُونَ

“Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito, hao ndio wenye kufaulu. Na yule ambaye mizani yake itakuwa khafifu, basi hao ni wale ambao wamekhasirika nafsi zao watakuwa katika [Moto wa] Jahannam ni wenye kudumu.” (23:102-103)

Kadhalika kunaingia kuamini uombezi katika kisimamo hicho. Kuna aina nne za uombezi:

1- Uombezi mkubwa. Huu ni kwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) peke yake na itapitika pindi watu wanasubiri wahukumiwe.

2- Uombezi ili milango ya Peponi ifunguliwe. Aina hii pia ni kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) peke yake.

3- Uombezi wa kukhafifishiwa adhabu kwa yule mwenye kuiistahiki. Kadhalika aina hii ni kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) peke yake pindi atapomuombea ami yake Abu Twaalib akhafifishiwe adhabu ya Moto. Haya ni malipo kwa kuwa alikuwa akimlinda na kumchunga.

4- Uombezi ili baadhi ya watu zinyanyuliwe daraja zao Peponi. Aina hii imesemekana kuwa ni kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) peke yake na imesemekana pia kuwa si yeye pekee.

5- Uombezi kwa wenye madhambi makubwa. Hawa ni wale wapwekeshaji watenda madhambi. Wametumbukia Motoni kwa sababu ya madhambi yao na wataombewa ili watoke humo. Uombezi huu Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Mitume na Malaika na waja wema wana haki juu yake.

Kadhalika Qur-aan na swawm vitawaombea watu wake siku ya Qiyaamah. Vilevile watoto wa waumini watawaombea wazazi wao.

Vilevile inahusiana na kuamini hodhi ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Maji yake ni maeupe kushinda maziwa, matamu kushinda asali na yenye harufu nzuri kushinda ya miski. Atayekunywa humo mara moja, basi hatohisi kiu tena kamwe.

Ni lazima pia kuamini Njia itayowekwa juu ya Moto. Watu watapita juu yake kwa mujibu wa matendo yao. Mtu wa kwanza atapita kama umeme, halafu kama upepo na halafu mwingine kama ndege. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesimama kwenye Njia akisema:

“Ee Mola! Salimisha, salimisha!”

Baada ya hapo matendo ya waja yatapungua mpaka atapokuja mtu ambaye atatambaa kwa sababu hawezi kutembea. Kwenye ncha ya Njia kumetundikwa ndoano zilizoamrishwa kumchukua wenye wastahiki. Hivyo mwenye furaha ataokoka na mla hasara atatumbukia Motoni.

Tunaamini yale yote yaliyokuja katika Qur-aan na Sunnah juu ya siku hiyo na hali zake – Allaah atulinde nazo.

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Mu´taqad as-Swahiyh, uk. 53-57
  • Imechapishwa: 21/06/2020