05. Hadiyth “Bwana mmoja katika Answaar alihudhuria kifo akasema… “

301 – Sa´iyd bin al-Musayyab (Radhiya Allaahu ´anh)[1] amesema:

:حَضَرَ رجلاً من الأنصار الموتُ فقال: إني محدثُكم حديثاً ما أحدثُكموه إلا احتساباً، سمعت رسول الله – صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ – يقول

“إذا توضّأَ أحدُكم فأحسَن الوضوءَ، ثم خرج إلى الصلاة، لم يرفعْ قَدَمَه اليمنى؛ إلا كَتَبَ الله عز وجل له حسنةً، ولم يضع قدمَه اليسرى؛ إلا حطَّ الله عز وجل عنه سيئة، فليُقَرِّبْ أحدكم أو ليُبَعِّدْ، فإن أتى المسجد فصلّى في جماعة غُفرِ له، فإن أتى المسجد وقد صلّوا بعَضاً وبقي بعضٌ؛ صلَّى ما أدرك، وأتم ما بقي كان كذلك، فإنْ أتى المسجد وقد صلَّوا فأتم الصلاةَ كان كذلك

“Bwana mmoja katika Answaar alihudhuria kifo akasema: “Mimi nitakuelezeni jambo, na sifanyi hivo isipokuwa ni kwa sababu ya kutaraji malipo. Nilimsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema: “Akitawadha mmoja wenu na akaufanya vyema wudhuu´, kisha akatoka kwenda kuswali, basi hatonyanyua mguu wake wa kulia isipokuwa Allaah (´Azza wa Jall) humwandikia tendo jema, hatoweka chini mguu wake wa kushoto isipokuwa Allaah (´Azza wa Jall) atamfutia dhambi. Kwa hiyo awe karibu mmoja wenu au awe mbali. Anapofika msikitini akaswali katika mkusanyiko, anasamehewa. Ikiwa atafika msikitini na akakuta wamekwishaswali sehemu ya swalah na kumebaki sehemu nyingine, basi ataswali kile alichowahi na atakamilisha kile kilichobaki. Akifika msikitini akakuta wameshaswali ambapo akakamilisha swalah, mambo yanakuwa vivyo hivyo.”[2]

Ameipokea Abu Daawuud.

[1] Sa´iyd bin al-Musayyab alikuwa ni mwanafunzi wa Maswahabah. Kitendo cha mtunzi wa kitabu kumtakia radhi kinaweza kumfanya msomaji kufikiri kwamba alikuwa Swahabah.

[2] Nzuri kupitia zingine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/241)
  • Imechapishwa: 02/12/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy