07. Hadiyth “Hakuna yeyote katika nyinyi atayetawadha… “

303 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

لا يتوضّأ أحدُكم فيُحسنُ وُضوءه فيُسبغه، ثم يأتي المسجدَ لا يريدُ إلا الصلاةَ فيه، إلا تَبَشْبَشَ الله إليه، كما يتبشبش أهلُ الغائب بطلعته

“Hakuna yeyote katika nyinyi atayetawadha, akaufanya vizuri na kueneza wudhuu´ wake, kisha akaenda msikitini na hakuna kingine alichokusudia isipokuwa kuswali humo, isipokuwa Allaah humfurahikia kama vile familia ya mtu asiyekuwepo wanavyofurahi pindi anapoonekana.”[1]

Ameipokea Ibn Khuzaymah katika “as-Swahiyh” yake.

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/242)
  • Imechapishwa: 02/12/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy