302 – Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

أتانى الليلة آت من ربى. وفي رواية: ربى في أحسن صورةٍ، فقال لى يا محمد، قلت: لبيك ربى وسعديك، قال: هل تدرى  فيم يختصم الملأُ الأعلى؟ قلت: لا أعلم، فوضع يده  بين كتفى، حتى وجدت بردها بين ثدي، أو قال في نحرى، فعلمت ما في السموات وما فى الأرض، أو قال ما بين المشرق والمغرب، قال: يا محمد أتدرى فيم يختصم الملأ الأعلى؟ قلت: نعم، في الدرجات، والكفارات ونقل الأقدام  إلى الجماعات، وإسباغ الوضوء في السبرات وانتظارالصلاة بعد الصلاة، ومن حافظ عليهن عاش بخيرٍ، ومات بخيرٍ، وكان من ذنوبه كيوم ولدته أمه

“Mola wangu alinijilia katika umbo zuri kabisa[1] na akasema: “Ee Muhammad! Unajua ni nini wanachobishana wale walimwengu walioko juu?” Nikasema: “Ndio. Ni kuhusu ngazi, kafara, hatua kuzienea swalah za mkusanyiko, kukamilisha wudhuu´ wakati wa baridi kali, kusubiri swalah baada ya swalah nyingine na yule ambaye atazihifadhi ataishi kwa kheri na atakufa kwa kheri na atasafishwa na dhambi zake kama siku ile aliyozaliwa na mama yake.”[2]

Ameipokea at-Tirmidhiy ambaye amesema:

“Hadiyth ni nzuri.”

[1] Ujio huu ilikuwa usingizini.

[2] Swahiyh kupitia zingine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/242)
  • Imechapishwa: 02/12/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy