08. Hadiyth “Kulikuwa kuna maeneo ya wazi pambizoni na msikiti… “

304 – Jaabir (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“بلغني أنّكم تريدون أنْ تنتقلوا قُرْبَ المسجد”. قالوا: نعم يا رسول الله! قد أردنا ذلك، فقال: “يا بني سَلِمَةَ! ديارَكم؛ تُكتَبْ آثارُكم، ديارَكم؛ تُكْتَبْ آثارُكم”. فقالوا: ما يسرنا أنَّا كنَّا تحولنا

“Kulikuwa kuna maeneo ya wazi pambizoni na msikiti ambapo Banuu Salamah wakataka kuhamia karibu na msikiti. Khabari hiyo ikamfikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo akawaambia: “Nimefikiwa na khabari ya kuwa mnataka kuhamia karibu na msikiti.” Wakasema: “Ndio, ee Mtume wa Allaah. Tumetaka kufanya hivo.” Akasema: “Ee Banuu Salamah, bakini katika majumba yenu!” Zinaandikwa nyayo zenu. Bakini katika majumba yenu!” Zinaandikwa nyayo zenu.” Wakasema: “Tusingelifurahishwa tungekuwa tumehama.”[1]

Ameipokea Muslim na wengineo. Imekuja katika tamko lingine:

إنَّ لكم بكل خُطوةٍ درجةً

“Hakika mna nyinyi kwa kila hatua mnayopiga ngazi.”

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/242-243)
  • Imechapishwa: 02/12/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy