09. Hadiyth “Answaar nyumba zao zilikuwa mbali na msikiti… “

305 – Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

:كانت الأنصارُ بعيدةً منازِلهم من المسجد، فأرادوا أنْ يقتَربوا، فنزلتْ

“Answaar nyumba zao zilikuwa mbali na msikiti ambapo wakataka kuhama karibu. Ndipo kukateremka:

وَكُلَّ شَيْءٍ أَحْصَيْنَاهُ فِي إِمَامٍ مُّبِينٍ

“Kila kitu Tumekirekodi barabara katika kitabu kinachobainisha.”[1]

Ndipo wakabaki katika maeneo yao[2].

Ameipokea Ibn Maajah kwa cheni ya wapokezi nzuri.

[1] 36:12

[2] Swahiyh kupitia zingine kutoka kwa Swahabah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/243)
  • Imechapishwa: 02/12/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy