10. Hadiyth “Kila ambavyo mtu anakuwa mbali zaidi na msikiti… “

306 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

الأبعدُ فالأبعدُ من المسجد أعظمُ أجراً

“Kila ambavyo mtu anakuwa mbali zaidi na msikiti, ndivo ujira wake unakuwa mkubwa zaidi.”[1]

Ameipokea Ahmad, Abu Daawuud, Ibn Maajah na al-Haakim aliyesema:

“Hadiyth ni Swahiyh. Wote walioko katika cheni ya wapokezi ni kutokea Madiynah.”

[1] Swahiyh kupitia zingine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/243)
  • Imechapishwa: 02/12/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy