3 – Swawm inaharibika kwa nia. Mwenye kunuia kufungua swawm yake anafungua na inaharibika swawm yake kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi ya wanazuoni. Kwani swawm ni ´ibaadah na miongoni mwa sharti zake ni kuweka nia katika sehemu zote za ´ibaadah. Akinuia kuikata basi ´ibaadah inaharibika kwa nia kutoka kwake nje na unaondoka ule uhakika wa ´ibaadah na hukumu yake. Katika hali hiyo inaharibika swawm yake kwa kuondoka sharti yake kutokana na yaliyotangulia:

“Hakika hapana vyenginevyo matendo yanategemea nia na kila mmoja atalipwa vile alivyonuia.”[1]

Matendo yanajengeka juu ya nia na matendo yanazingatiwa kwayo. Nia ndio inayosahihisha ´ibaadah na ´ibaadah ni yenye kuzungukia juu ya nia.

Swalah na amani zimwendee Mtume wetu Muhammad, kizazi chake na Maswahabah wote.

[1] al-Bukhaariy (01) na Muslim (1907).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus fiy Ramadhwaan, uk. 14
  • Imechapishwa: 11/04/2023