03. Kulala na nia juu ya swawm ya faradhi

2 – Si sahihi kufunga swawm ya faradhi isipokuwa kwa kulaza nia usiku. Imethibiti kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba amesema:

“Ambaye hakuazimia swawm kabla ya Fajr, basi hana swawm.”[1]

Imekuja katika tamko jingine:

“Ambaye hakulaza swawm kabla ya Fajr, basi hana swawm.”[2]

Imekuja katika tamko jingine:

“Ambaye hakulaza swawm sehemu ya usiku, basi hana swawm.”[3]

Imethibiti vilevile kwa al-Bukhaariy na Muslim ambao wamepokea kupitia kwa ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye ameeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika hapana vyenginevyo matendo yanategemea nia na kila mmoja atalipwa vile alivyonuia.”[4]

[1] Abu Daawuud (2454).

[2] an-Nasaa´iy (2331).

[3] an-Nasaa´iy (2334).

[4] al-Bukhaariy (01) na Muslim (1907).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus fiy Ramadhwaan, uk. 14
  • Imechapishwa: 11/04/2023