Swali: Je, niswali Witr baada ya swalah ya ´Ishaa Rak´ah tatu au Rak´ah moja?

Jibu: Witr ni kutokana na vile inavowepesika; Rak´ah tatu, tano, saba au tisa. Haina kikomo maalum safarini wala katika hali ya ukazi. Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiswali Witr safarini na katika hali ya ukazi. Vivyo hivyo kuhusu Sunnah ya Witr katika hali zote mbili ya usafiri na ukazi. Kuhusu Sunnah ya Dhuhr, ´Aswr, Maghrib na ´Ishaa wakati wa safari bora ni kuziacha.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/48)
  • Imechapishwa: 11/04/2023