04. Hadiyth ”Yule mwenye kukuswalia mara moja… ”

4 – ´Abdullaah bin Maslamah ametuhadithia: Salamah bin Wardaan ametuhadithia: Nimemsikia Anas bin Maalik akisema:

خرج النبي صلى الله عليه وسلم يتبرز، فلم يجد أحداً يتبعه، فهرع عمر فاتبعه بمطهرة – يعني إداوة – فوجده ساجداً في شَرَبةَ  فتنحى عمر فجلس وراءه حتى رفع رأسه قال: فقال: (أحسنت يا عمر حين وجدتني ساجداً فتنحيت عني، إن جبريل عليه السلام أتاني فقال: من صلى عليك واحدة صلى الله عليه عشراً، ورفعه عشر درجات).

”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitoka kwenda kufanya haja. Hakumpata yeyote wa kumfuata, ´Umar akamkimbilia na chombo cha maji. Akamkuta amesujudu katika ardhi yenye nyasi. ´Umar akaenda kando na akaketi nyuma yake mpaka aliponyanyua kichwa chake. Akasema: ”Umefanya vizuri, ee ´Umar, wakati uliponiona nimesujudu ambapo ukajitenga mbali nami. Jibriyl (´alayhis-Salaam) amenijia na akasema: ”Yule mwenye kuniswalia mara moja, basi Allaah atamswalia mara kumi  na atamnyanyua ngazi kumi.”[1]

[1] Cheni ya wapokezi wake ni dhaifu, lakini maneno  yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni Swahiyh na yanatiliwa nguvu kupitia njia nyingi.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 25-26
  • Imechapishwa: 29/01/2023