03. Hadiyth ”Yule mwenye kuniswalia mara moja… ”

3 – Ishaaq bin Muhammad al-Farwiy ametuhadithia: Abu Twalhah al-Answaariy ametuhadithia, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Ishaaq bin ´Abdillaah bin Abiy Twalhah, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa baba yake ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Alalah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

من صلى عليَّ واحدة صلى الله عليه عشراً، فليكثر عدد ذلك، أو ليقلّ

”Yule mwenye kuniswalia mara moja, basi Allaah atamswalia mara kumi. Hebu mwache akithirishe idadi yake au afanye kwa uchache.”[1]

[1] Cheni ya wapokezi wake ni dhaifu kwa sababu ya al-Farwiy. ad-Duulaabiy  amesema katika “al-Kunaa” ya kwamba huyu Abu Twalhah anaitwa ´Abdullaah bin Hafsw. Ibn Abiy Haatim amemtaja katika “al-Jarh wat-Ta´diyl” pasi na kumjeruhi wala kumsifu. Wala sikutaja taarifa yoyote kuhusu baba yake Hafsw. Hadiyth inatiwa nguvu na Hadiyth nyingine itayokuja huko mbele kwenye kitabu. Pengine ikatiwa nguvu nayo. Isitoshe al-Mundhiriy amesema kuwa ni nzuri, kama itakavyokuja huko mbele.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 25
  • Imechapishwa: 29/01/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy