02. Hadiyth ”Siku moja Mtume wa Allaah alikuja na bashasha inaonekana usoni mwake… ”

2 – Sulaymaan bin Harb ametuhadithia: Hammaad bin Salamah ametuhadithia, kutoka kwa Thaabit al-Bunaaniy, kutoka kwa Sulaymaan, mtumwa wa al-Hasan bin ´Aliy aliyemwacha huru, kutoka kwa ´Abdullaah bin Abiy Twalhah, kutoka kwa baba yake ambaye amesema:

أن رسول الله صلى الله عليه وسلم جاء يوماً والبشر يرى في وجهه، فقالوا: يا رسول الله إنا نرى في وجهك بشراً لم نكن نراه، قال: (أجل إنه أتاني ملك فقال: يا محمد إن ربك يقول: أما يرضيك ألا يصلي عليك أحد من أمتك إلا صليت عليه عشراً، ولا سلّم عليك إلا سلمت عليه عشراً).

”Siku moja Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuja na bashasha inaonekana usoni mwake. Wakasema: ”Ee Mtume wa Allaah, hakika sisi tunaona furaha usoni mwako ambayo tulikuwa hatuioni kabla.” Akasema: ”Ni kweli. Amenijia Malaika akasema: ”Ee Muhammad! Hakika Mola wako anasema: ”Je, haikupendezi kwamba hakuna yeyote katika ummah wako ambaye anakuswalia, isipokuwa namswalia mara kumi, na hakutakii amani, isipokuwa na mimi namtakia amani mara kumi?”[1]

[1] Hadiyth ni Swahiyh ikijumuisha ilio kabla yake na ilio baada yake. Ni Swahiyh kwa mujibu wa Ibn Hibbaan (2391).

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 24-25
  • Imechapishwa: 29/01/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy