01. Hadiyth ”Siku moja Mtume wa Allaah alitutokea…. ”

1 – Ismaa´iyl bin Abiy Uways ametuhadithia: Ndugu yangu amenihadithia, kutoka kwa Sulaymaan bin Bilaal, kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Umar, kutoka kwa Thaabit al-Bunaaniy: Anas bin Maalik amesema: Abu Twalhah amesema:

أن رسول الله صلى الله عليه وسلم جاء يوماً والبشر يرى في وجهه، فقالوا: يا رسول الله إنا نرى في وجهك بشراً لم نكن نراه، قال: (أجل إنه أتاني ملك فقال: يا محمد إن ربك يقول: أما يرضيك ألا يصلي عليك أحد من أمتك إلا صليت عليه عشراً، ولا سلّم عليك إلا سلمت عليه عشراً).

”Siku moja Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitutokea. Kulionekana bashasha usoni mwake. Wakasema: ”Hivi sasa tunajua furaha usoni mwako, ee Mtume wa Allaah!” Akasema: ”Ni kweli. Amenijia mwenye kunijia kutoka kwa Mola wangu akanieleza kuwa hakuna yeyote katika ummah wangu atakayeniswalia, isipokuwa Allaah atamrudishia mara kumi.”[1]

[1] Ahmad, an-Nasaa’iy na Ibn Hibbaan katika “as-Swahiyh”. Swahiyh kupitia njia zake zote. Mtunzi ameipokea kupitia njia mbili na kuna yenye kuitia nguvu kutoka kwa Anas na nyingine kutoka kwa ´Umar.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 23-24
  • Imechapishwa: 29/01/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy