05. Hadiyth ”Yule mwenye kukuswalia mara moja… ”

5 – Ya´quub bin Humayd amenihadithia: Anas bin ´Iyaadhw amenihadithia, kutoka kwa Salamah bin Wardaan: Maalik bin Aws bin al-Hadathaan amenihadithia, kutoka kwa ´Umar bin al-Khattwaab, ambaye amesema:

خرج النبي صلى الله عليه وسلم يتبرز، فاتبعه بإداوة، فوجدته قد فرغ، ووجدته ساجداً لله في شَربَة، فتنحيت عنه، فلما فرغ، رفع رأسه فقال: (أحسنت يا عمر حين تنحيت عني، إن جبريل أتاني فقال: من صلى عليك صلاة، صلى الله عليه عشراً، ورفعه عشر درجات).

”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitoka kwenda kufanya haja. Nikamfuata na chombo cha maji na nikamkuta amemaliza. Nikamkuta amemsujudia Allaah kwenye ardhi yenye nyasi. Hivyo nikaenda kando naye. Alipomaliza alinyanyua kichwa chake na akasema: ”Umefanya vizuri, ee ´Umar, wakati ulipojitenga mbali nami. Hakika Jibriyl amenijia na akasema: ”Yule mwenye kukuswalia mara moja, basi Allaah atamswalia mara kumi  na atamnyanyua ngazi kumi.”[1]

[1] Cheni ya wapokezi wake ni dhaifu, lakini yanasemwa juu yake yale yanayosemwa katika kuhusu ile Hadiyth ya kabla yake.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 25
  • Imechapishwa: 29/01/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy