06. Hadiyth ”Hakuna mja yeyote anayeniswalia… “

6 – ´Aaswim bin ´Aliy amenihadithia: Shu´bah bin al-Hajjaaj amenihadithia, kutoka kwa ´Aaswim bin ´Ubaydillaah bin ´Aamir bin Rabiy´ah, kutoka kwa baba yake, ambaye amesimulia kuwa amemsikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

ما من عبد يصلي عليَّ إلا صلت عليه الملائكة ما صلى علي، فليقل من ذلك أو ليكثر

”Hakuna mja yeyote anayeniswalia, isipokuwa Malaika humswalia muda wa kuwa ananiswalia. Hebu mwache akithirishe idadi yake au afanye kwa uchache.”[1]

[1] Cheni ya wapokezi ni dhaifu. Ahmad, Ibn Abiy Shaybah, Ibn Maajah na wengineo kupitia kwa ´Aaswim bin ´Ubaydillaah. al-Mundhiriy amesema:

”Hata kama ´Aaswim ni mnyonge katika kusimulia Hadiyth, baadhi wamempitisha. Miongoni mwa waliyosahihisha upokezi wake ni at-Tirmidhiy. Hadiyth hii ni nzuri kupitia zingine – na Allaah ndiye anajua zaidi.” (at-Targhiyb wat-Tarhiyb (2/280))

Miongoni yanayoitia nguvu ni Hadiyth ya tatu. Kisha nikapata kuwa Abu Nu´aym ameipokea kutoka kwa mpokezi mwingine katika “Hilyat-ul-Awliyaa’” (1/180). Angalau kwa uchache Hadiyth ni nzuri.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 27
  • Imechapishwa: 29/01/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy