07. Hadiyth ”Yule mwenye kukuswalia, basi nami nitamswalia… ”

7 – Yahyaa bin ´Abdil-Hamiyd ametuhadithia: ´Abdul-´Aziyz bin Muhammad ametuhadithia, kutoka kwa ´Amr bin Abiy ´Amrah, kutoka kwa ´Abdul-Waahid bin Muhammad, kutoka kwa ´Abdir-Rahmaan bin ´Awf, ambaye amesema:

أتيت النبي صلى الله عليه وسلم وهو ساجد فأطال السجود، قال: (أتاني جبريل قال: من صلى عليك صليت عليه، ومن سلم عليك سلمت عليه، فسجدت لله شكراً

”Nilimwendea Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kumkuta amesujudu ambapo amerefusha sujuud. Kisha akasema: ”Jibriyl amenijia na akasema: ”Yule mwenye kukuswalia, basi nami nitamswalia, na mwenye kukutakia amani, basi nami nitamkia amani.” Ndipo nikamsujudia Allaah kumshukuru.”[1]

[1] Hadiyth ni Swahiyh kwa njia zake na mapokezi yanayoitia nguvu. Ameipokea Ahmad na al-Haakim, ambaye amesema:

”Cheni ya wapokezi wake ni Swahiyh.”

Imepokelewa kwa njia nyingine (10).

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 27
  • Imechapishwa: 29/01/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy