Kuhusu vita vya kujihami, kwa mfano mtu amekuvamia nyumbani na anataka kuchukua mali yako au anataka kumnajisi mke wako, mpige vita kama alivokuamrisha kufanya hivo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Aliulizwa juu ya mtu mwenye kumjia na kumwambia: “Nipe mali yako.” Akasema (´alayhis-Salaam): “Usimpe.” Akauliza: “Unaonaje akinipiga vita?” Akasema: “Nawe mpige vita.”Akauliza: “Unaonaje aniniua?” Akasema: “Akikuua basi wewe ni shahidi.” Akauliza: “Unaonaje ikiwa mimi ndiye nitamuua?” Akasema: “Ukimuua basi yeye ataingia Motoni.”[1]

Kwa sababu ni mvuka mipaka na mwenye kudhulumu. Haijalishi kitu hata kama itakuwa ni muislamu.

Akija muislamu na kutaka kukupiga vita utoke katika mji wako au nyumbani kwako, mpige vita. Ukimuua anaingia Motoni. Akikuua basi wewe ni shahidi. Usihoji ni vipi nitamuua muislamu? Huyu ni mvuka mipaka.

[1] Muslim (140)

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/67)
  • Imechapishwa: 29/01/2023