Ndio maana swalah ya mkusanyiko ni lazima

Maoni yenye nguvu miongoni mwa maoniya wanachuoni ni kwamba swalah ya mkusanyiko ni faradhi kwa kila mtu. Ni wajibu kwa mwanaume kuswali na mkusanyiko msikitini kutokana na Hadiyth zilizothibiti juu ya hilo na yale aliyoashiria Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) katika Kitabu Chake:

وَإِذَا كُنتَ فِيهِمْ فَأَقَمْتَ لَهُمُ الصَّلَاةَ فَلْتَقُمْ طَائِفَةٌ مِّنْهُم مَّعَكَ 

“Utapokuwa upo kati yao ukawaswalisha, basi lisimame kundi miongoni mwao pamoja nawe.” (04:102)

Allaah amewajibisha kuswali mkusanyiko katika hali ya khofu. Ikiwa ameiwajibisha katika hali ya khofu, basi katika hali ya amani ni aula zaidi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/73)
  • Imechapishwa: 29/01/2023