03. Bora kuwa muwastani juu ya uongofu kuliko mwenye bidii juu ya upotevu

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

“Mwenendo wa kipindi cha kikafiri inahusu kila kitu cha kipindi cha kikafiri, kisichofungwa au kisichokufungamana kwa mtu kama myahudi, mnaswara, mwabudia sanamu au mwingine mwenye kwenda kinyume na yale waliyokuja nayo Mitume.”[1]

al-Bukhaariy amepokea kutoka kwa Hudhayfah ambaye amesema:

“Enyi wanazuoni! Bakieni katika njia iliyonyooka! Mkifanya hivo basi hakika mtakuwa mmetangulia mbele. Na mkienda kuliani na kushotoni basi hakika mmepotea upotevu wa mbali kabisa.”[2]

MAELEZO

Maana ya nyookeeni bi maana bakieni juu ya njia. Wasomaji wanakusudiwa wanazuoni na wanafunzi. Anachotaka kusema ni kwamba kuweni na msimamo juu ya dini ya Allaah. Mja anaponyooka basi hakika ametangulia mbele kabisa. Anaposhika njia za kuliani na kushotoni, basi kwa hakika amepotea upotofu wa mbali kabisa. Kilicho cha lazima ni mtu kushikmana na yale Allaah aliyoweka katika Shari´ah na kujiepusha na yale aliyoyasema vibaya:

أَمْ لَهُمْ شُرَكَاءُ شَرَعُوا لَهُم مِّنَ الدِّينِ مَا لَمْ يَأْذَن بِهِ اللَّـهُ

“Je, wanao washirika wanaowatungia Shari´ah yale ambayo Allaah hakuyaidhinisha?” (42:21)

Baki juu ya njia ilionyooka, japo ni mwenye kufanya ´ibaadah kwa wastani pamoja na wema walio kati kwa kati, ni bora kuliko kufuata njia zilizopotea kutokamana na uongofu. Kwa sababu zinawapotosha na kuwaweka mbal ina Allaah (´Azza wa Jall). Bali mtu ambaye anafuata uongofu, ingawa ataidhulumu nafsi yake kwa kutenda baadhi ya maasi, yuko juu ya njia ya uokozi. Lakini yule mwenye kufuata njia ilio kinyume na Uislamu na akataka kuleta katika Uislamu mwenendo wa kipindi cha kikafiri yuko katika njia angamivu. Tunamuomba Allaah afya na usalama.

[1] Iqtidhwaa´-us-Swiraat al-Mustaqiym (01/79).

[2] al-Bukhaariy (7282).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fadhwl-il-Islaam, uk. 09-10
  • Imechapishwa: 08/10/2020