02. Sababu nne za ubora wa kufunga swawm ya Shawwaal kwa kufululiza

Bora ni mtu kufunga siku sita hizi kwa kufuatanisha ingawa inafaa kuziachanisha muda wa kuwa ni ndani ya mwezi. Kuzifunga mara tu baada ya ´Iyd-ul-Fitwr kumalizika kuna sifa za kipekee kuliko kuzifunga kwa kuachanisha. Hilo ni kwa njia nyingi:

1 –  Kufanya hivo kuna kuharakia kufanya mambo ya kheri.

2 – Mtu kuziharakisha ni alama ya shauku yake ya kufunga na kuonyesha kuwa haikumchosha.

3 – Asije kuzukiwa na kikwazo cha kuifunga endapo ataichelewesha.

4 – Kufunga siku sita baada ya Ramadhaan ni kama kuswali Raatibah baada ya swalah ya faradhi, jambo ambalo linakuwa baada yake. Allaah ndiye mjuzi zaidi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtaswar Ahaadiyth-is-Swiyaam, uk. 84-85
  • Imechapishwa: 08/03/2023